Inakimbizaaaaa


Friday, September 25, 2009

DIBANJI KUTUA DAR KWA AJILI YA MTV AFRICA MUSIC AWARDS


Msanii D'Banj kutoka Nigeria ambae anatamba na wimbo wake Fallin Love, anakuja Dar es Salaam tar 3 October kwa ajili ya show na baadae ataelekea Nairobi kwa ajili ya uwepo wake katika tuzo za MTV...
Kwa mengi zaidi tembelea mtvbase.com na pages mbali mbali za MTV kama facebook na twitter
Kutoka kwetu Tanzania tutawakilishwa na AY na SHAA

Thursday, September 24, 2009

WAANDAAJI WA MAISHA PLUS WAKUMBWA NA TUHUMA YA KUPOKEA HONGO


waandaaji wa kipindi cha televishen kinachojulikana kama maisha plus wamekumbwa na tuhuma ya kupokea hongo kutoka kwa mshindi wa kipindi hicho. kutokana na gazeti la DAILY NEWS waandaaji hao walimtaka mshindi kuwapatia milioni 3 katika milioni 10 aliyoshinda. Mmoja wa waandaaji hao masood kipanya amesema tuhuma hizo hazina maana yoyote na sishangai kuskia hili hasa wakati huu ambapo maisha plus ndio inaongezeka umaarufu.tuhuma hizi zinatoka kwa maadui tu ambao wanataka kuniharibia sifa yangu amesema kipanya.lakini wameendela kusema kuwa waandaaji hao waitoa offa hiyo kwa washiriki wengine lakini walikataa.mshindi wa maisha plus mwaka huu anatarajiwa kupata shilingi million 15 tofauti na mwakajana.

Wednesday, September 23, 2009

AY APOKELEWA KWA PART MALYASIA







Hizi ni Picha maalum za welcome Party aliyofanyiwa jana msanii AY kwenye Club ya HELO BALI mjini Kualar Lumpa, Malaysia. Show kamili inafanyika kesho tarehe 24 kwenye ukumbi wa TITUNIUM CLUB. Wabongo waishiyo Malaysia kazi kwenu kuona vitu vya 'nominee' wa MTV Africa Music Awards 2009!!!

HUYU NDIYE IRENE UWOYA WA UKWELI CHEKI MTOTO ALIVYOSIMAMA



Miss TZ & Talent show night ijumaa hii giraffe ocean view hotel


Warembo wa Miss TZ wakiwa katia uzi wa kutangaza utalii. Ijumaa September 25, 2009 watakuwa na Miss Tanzania Day & Talent Show night ambapo wadau wanakaribishwa Giraffe Ocean View hotel iliyopo Kunduchi kushuhudia warembo wakichuana katika shindano la vipaji mbalimbali walivyojaaliwa navyo kuanzia saa moja jioni. kiingilio ni alfu 40 kwa kichwa na mshindi wa shindano hilo atabeba laki 5 keshi.

Wednesday, September 16, 2009

UNAMFAHAMU LOVENESS LOVE (DIVA) WA CLOUDS FM ALA ZA ROHO SEASON 2

I can't believe the season Two of Keeping Up with the Diva is here already! It feels like the show just started!
Time flies so fast! The season is pretty intense. there is a lot of relationship drama in it this time via Clouds Fm Ala za Roho show witcha Diva Loveness Love.. Kuanzia nne kamili mpaka 6 kamili za usiku.. Everyday Jumatatu Mpaka Alhamis

http://www.diva255.com/

VIGGOGO WANNE WA BENKI KUU WAFIKISHWA MAHAKAMANI

VIGOGO wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 104 bilioni.

Vigogo hao ambao wote ni wakurugenzi wa BoT wa vitengo tofauti, walifikishwa mahakamani hapo asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Wameshtakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

Wakurugenzi hao wanashtakiwa kwa makosa tofauti ikiwamo kosa la tatu linalowahusisha wote wanne ambao ni Mkurugenzi wa Benki ya BoT, Simon Eliezer Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Kisima Thobias Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bosco Ndimbo Kimela na Mkurugenzi wa benki, Ally Farijallah Bakari.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincon alimwambia hakimu Samuel Maweda kuwa vigogo hao wanne, wakiwa watumishi wa umma walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kuisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146.

“Kwa pamoja na kwa makusudi walishindwa kuchukua tahadhari au kusahau majukumu yao katika mazingira nyeti, kwa udanganyifu walitayarisha nyongeza kwenye mkataba wa 2001 unaohusiana na uchapaji wa noti za benki kwa gharama kubwa ambapo bei ya mkataba huo iliisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146,” alidai Licon.

Licon aliendelea kuieleza mahakama kuwa mwaka 2004 washtakiwa Jengo na Mkango wakiwa ndani ya jiji na Mkoa wa Dar es Salaam na wakiwa wameajiriwa katika utumishi wa umma katika nyadhifa tofauti ndani ya BoT, kwa pamoja na kwa makusudi, wakiwa na lengo la kuvunja kanuni walitangulia kutoa ofa kwa wasambazaji wa noti za benki.Pauline Richard na Salim Said

Monday, September 14, 2009

INASADIKIKA KUWA MPAKANJIA AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa mume wa marehemu Amina Chifupa,Mohamed Mpakanjia amefariki leo mnamo majira ya saa tisa ,jioni hii katika hospitali ya jeshi ya Lugalo,Inaelezwa kuwa Mpakanjia alikuwa amelazwa hospitalini hapo toka juzi akisumbuliwa na ugonjwa wa Neumonia.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN

HUYU NDIE RAY BWANA (FATAKI) MZEE WA ATM...... ALL STAR

Wandugu nawatangulizia movie nyingine hiyo ambayo iko jikoni inapikwa "Fair Decision" itatoka soon baada ya "Divorce" ambayo itakuwa madukani kuanzia tarehe 29/9/2009. sina mengi saana itakapotoka pata nakala yako. Mdau Ray.
kwa picha na habari kibao
za tasnia ya filamu bongo

MUZIKI BASI MPAKA MWAKANI NIMALIZE SHULE (NOORAH)

Noorah aka The Babaz of The Mamaz amelonga na Bongo Star Link na kusema kwa sasa elimu kwake ikiwa imefikia mkiani kwa Ng'ombe, ameona awaambie mashabiki wake wawe na subira kidogo mpaka hapo mwakani mwezi wa 6.
Kwa kipindi hicho chote basi amesema mashabiki wake wanaompenda wanaweza kuchukua simu zao za mkononi na kwenda sehemu ya sms na kuandika

BABAZ kwenda 15327 au NOORAH kwenda 15551.

Hapo wataweza kuwasiliana na yeye moja kwa moja kwenye simu yake ya mkononi na yeye atakuwa anawafahamisha habari mpya kuhusu maendeleo yake, it's means wao ndio watakuwa wa kwanza kujua before anyone

HUYU NDIE MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA BIG BROTHER AFRICA4

Elizabeth
Age 21
Country Tanzania
Hometown Dar Es Salaam
Occupation TV Presenter / Actress
Biography Elizabeth has one sister, two brothers and she's a Miss Tanzania Top 10 finalist. She says the best part of her country to visit is Mount Kilimanjaro and the best thing about Tanzanians is their kind and positive nature. Elizabeth is a big Man United and Chicago Bulls fan and rates sleeping late and waking up too early as her bad habits. She loves dancing, needle work, cooking, watching TV and traveling - she has also lived in Hungary.

Saturday, September 12, 2009

MASIKINI WEMA SEPUTU

Mazoea yana tabu, msemo huo upo nyuma ya adha anayoipata hivi sasa, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kutokana na jinsi anavyohangaikia gari za kukodi wakati amezoea ‘kusumbua’ kwa usafiri wake binafsi....

Friday, September 11, 2009

AMBWENE YESAYA KUTUMBUIZA JUMAPILI HII BIG BROTHER AFRICA

Ambwene Yesaya (ay)
habari zimeingia punde zinadatisha kwamba mwanamuziki nyota wa kizazi kipya ambwene yesaya a.k.a AY anaondoka Jumamosi hii kuelekea sauzi katika jiji la johannesburg ambako atatumbuiza kwenye hafla ya Big Brother. Ataongozana na Snare wa east coast.
AY kaiambia globu ya jamii kwa njia ya twitter sasa hivi kwamba yeye kama kawaida yake hana show kubwa wala ndogo na kwamba show zote kwake ni muhimu hivyo anajiandaa kwa makamuzi ya nguvu.
kasema baada ya sauzi ataelekea Malaysia ambako atakuwa na show jijini Kuala lumpur September 24, mwaka huu ndani ya klabu cha Titunium. Pia ataporejea wiki ijayo anatarajiwa kutoa singo ingine mpya iitwayo 'Bed & Breakfast' ambayo imetayarishwa na Hermy B wa B. Hitz Studios.
Wakati huo huo AY anawakumbusha wadau wote popote walipo hapa bongo kumpa taffu kwa kumpigia kura katika tuzo za Mtv Africa. Kumpigia kura andika 'BHH AY' kisha tuma sms kwenda namba 0789 777 333

BONGO CELEBRIT YAKATA MZIZI WA FITINA


kutokana na madongo anayorushiwa supa staa steven kanumba kwa kile kinachodaiwa kuchapia kiinglishi,
WWW.BONGOCELEBRIT.COM
ambayo ni globu dada ya globu ya jamii, imeandaa clip za baadhi ya matukio katika jumba la Big Brother Africa IV akiwemo kanumba ili kukata mzizi wa fitna. ili kuona kama hayo yasemwayo ni kweli ama uzushi....
BOFYA HAPA

Thursday, September 10, 2009

TID KUSHUKA NA FILAMU YAKE INAYOELEZEA MAISHA YA JELA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava, Khalid Mohamed aka 'TID' anarejea tena kwenye medani ya filamu na kutoka na filamu yake ya Prisoner inayozungumzia maisha yake ya gerezani.
Akizungumza hivi karibuni, TID anayemiliki bendi ya Top Band, alisema kuwa ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuweka hadharani maisha wanayoishi wafungwa wawapo gerezani.

TID alifungwa kifungo cha mwaka mmoja mwaka jana kutokana na kosa la kumjeruhi mtu akiwa klabu, lakini aliweza kutoka jela kutokana na msamaha wa rais mwishoni mwa mwaka jana.

Mwanamuziki huyo ambaye amebadilika kitabia mara baada ya kutoka jela, alisema kuwa amejifunza mambo mengi alipokuwa gerezani na anahitaji kutoa elimu kwa wananchi.

"Kule gerezani nimekutana na mambo mengi yanayotisha na yanayokwenda kinyume na haki za binadamu. Nimeona kuna haja ya kuandaa filamu hii, ili wengine ambao hawajawahi kwenda jela waweze kujifunza," alisema mwanamuziki huyo.

TID ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliotoa mchango mkubwa katika medani ya filamu, hasa kutokana na ushiriki wake katika filamu ya Girl Friend, ambayo ilitoa hamasa kubwa kwa watanzania kushiriki filamu.

UNAWAJUA MAPACHA HAWA WAKO NDANI YA BBA 4


Shindano la nne la Big Brother limeanza jana jijini Johannesburg kwa mbwembwe za hali ya juu huku mabadiliko makubwa yakijitokeza kama kauli mbiu yao "mapinduzi" isemavyo.

Moja ya vivutio vikubwa katika uzinduzi wa shindano hilo ni pamoja na uhusishwaji wa mastaa wa tasnia ya filamu barani Afrika ambapo msanii Kanumba wa Tanzania aliungana na mastaa wengine watatu katika jumba hilo kuwakaribisha washiriki 11 kati ya washiriki 14 wanaotakiwa katika nyumba hiyo.
Moja ya mambo yaliyostua wadau na wapenzi wengi wa shindano hilo la Big Brother Revolution 2009 ni pamoja na kutoingia kwa washindani 3 wa nchi za Tanzania, Angola na Zambia kitendo kilichotafsiriwa na wengi ya kuwa huenda Kanumba ndiye mshiriki kamili wa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo meneja masoko wa kampuni ya Multi Choice Tanzania aliwataka watanzania kuwa na subira ili kujua hatma ya ushiriki wao.

Uzinduzi huo ambao uliongozwa na MC mahiri kabisa IK kutoka nchini Nigeria ilipambwa na burudani toka kwa K'naan na pia ilikuwa na surprise ya washiriki mapacha kutoka Namibia pamoja na washiriki mmoja mmoja zaidi kutoka Kenya na Uganda.
Aidha washiriki wote 12 walioingia ni wanaume na waliobaki inasemekana ni wanawake hivyo kuweka shauku ya hali ya juu kwa watazamaji wa shindano hilo.

KWA HILI RAISI JAKAYA AMEANDIKA HISTORIA MPYA TANZANIA


Mh Rais Jakaya Kikwete akiongea moja kwa moja na wananchi kupitia Luninga na Redio kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Tido Muhando.
Hivi ndiyo ilivyokuwa wakati Rais Jakaya alipoongea na watanzania (Live) moja kwa moja kupitia Redio na Televisheni na kuulizwa maswali mbalimabli na wananchi ili kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa yahusuyo utendaji wa serikali na matarajio ya watanzania.
Utaratibu huu umebuniwa kwa mara ya kwanza na Rais Jakaya na ni kwa mara ya kwanza toka tujipatie uhuru kutoka kwa wakoloni, Mh Rais alizungumzia mengi na kujibu maswali mengi kutoka kwa wananchi
Lakini moja ya mambo aliyozungumzia ni uhuru wa wananchi kuzungumzia na kukosoa utendaji wa serikali na akazungumzia pia uhuru wa vyombo vya habari na kusisitiza vyombo hivyo kufuata maadili ya kazi zao bila kuandika habari za uongo na uchochezi, hili ni jambo jema sana kwani tunahitaji habari nyingi zaidi lakini pia tunahitaji habari za kweli na zenye upembuzi yakinifu ili jamii iweze kupata habari zilizo sahihi
Tunakupongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wako wa kuongea na wananchi huku ukiulizwa maswali mabalimbali na kuyajibu, kwa kutendo hiki umeandika historia mpya ya uhuru wa umma kupata habari na kutoa maoni yao juu ya uendeshaji na uboreshaji wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla tunakupa Heko kwa uamuzi wako huu na tunadhani utazaa matunda, tunakutakia mafanikio mema katika kazi zako za kila siku katika kujenga Taifa letu Tanzania.

Monday, September 7, 2009

KANUMBA MMOJA WA MASTAA WATAKAOWAKARIBISHA WASHIRIKI WA BIG BROTHER AFRICA 4

kanumba,mmoja wa mastaa atakayewakaribisha washiriki wa big brother africa 4 2009 ndani ya jumba lao
Muigizaji nyota wa filamu hapa bongo, Steven Charles Kanumba(pichani)amechaguliwa kuwa mmoja wa mastaa watakao wakaribisha washiriki wa shindano la Big brother afrika 4 ,2009 nchini afrika ya kusini.Kanumba ameukwaa ustaa huo baada ya kutajwa jana kwenye hafla fupi iliofayika pale Paradise City Hotel - Savanna Lounge jiji Dar,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi rasmi wa shindano hilo,iliyoandaliwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania.
Aidha muwakilishi wa shindano hilo kwa hapa Tanzania,imeelezwa kuwa atatangazwa hapo baadaye.Tanzania imeshafanikiwa kuwakilishwa na Mwisho Mwampamba, Richard ambaye alikuwa mshindi na Latoya.
BIG BROTHER AFRICA 2009
Hatimaye lile shindalo la big brother africa limeanza tena na anaonekana msanii kanumba ndani ya jengo lile wengi wanadhani labda yeye ndio mshiriki kutoka tanzania kumbe wala hata hausiki na chochote je unajua ni ni kanumba anachokifanya ndani ya jengo hilo tulia hapahapa nitakujuza na je unamjua mshiriki halali atakayeingia ndani ya shindalo hilo basi nitakuja mengi kuhusiana na hilo

Friday, September 4, 2009

HEBU TOA MAWAZO YAKO KUHUSU PICHA HIZI

NI NINI AY KAMAKAWA

Thursday, September 3, 2009

DOKII AIBUKA KWENYE FILAMU NA KUTESA TENA KATIKA BAD FRIEND
Wengi walikuwa walimtambua na wanaendelea kumtambua kwa jina la Dokii hasa kwa umahiri na umaarufu wake alokuwa nao katika fani ya uigizaji,kama mtakuwa mnakumbuka vyema alikuwa akiigiza katika mchezo wa mambo hayo kilichokuwa kinarushwa na telvisheni ya ITV wakati ule,Dokii akapotea kiasi na kujikita kwenye anga ya muziki wa injili kwa muda.Kwa sasa amerejea kwa kasi mpya katika fani yake ya ugizaji,kuhakikisha kuwa kipaji chake cha uigizaji bado kiko pale pale Dokii ameibuka kwenye filamu ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni iitwayo Bad Friends,humo ameonesha umahiri wake mkubwa katika kuucheza uhusika wake sawia.
Eritrea yawataja warembo wake wataoshiriki miss east africa 2009
Selamawit Zerabruck Ghebreslassie
Date of Birth 19-08-1991
Height 172
Hobbes reading, Traveling, movies

Sefora Messele Ghebreezgabiheir
Date of Birth 19-09-1991
Height 180Hobbies swimming, reading

Eritrea imekuwa nchi ya kwanza kutangaza warembo wake katika mashindano ya kimataifa ya urwembo ya Miss East Africa mwaka huu yatayofanyika December 18, 2009 jijini Dar. Warembo hao walipatikana katika mashindano ya kuvutia ya urembo yaliyofanyika jijini Asmara Nchini humo hivi karibuni.

Warembo watakaoiwakilisha Eritrea katika mashindano ya mwaka huu niSelamawit Zerabruck Ghebreslassie na Mesele Ghebreezgabiheir.Mwaka jana Nchi ya Eritrea pia ilikuwa ya kwanza kutangaza wawakilishi wake katika mashindano ya Miss East Africa 2008 yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ambapo iliwakilishwa na warembo Rahwa Ghebrehiwet pamoja ya Menal Hussien ambapo Rahwa Ghebrehiwet alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu.

Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa huandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar.Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, visiwa vya Seychelles, Re union, Madagascar, Comoros na Mauritius.

Wakati huohuo ile bahati nasibu ya Miss East Africa ya kuchangia yatima ambapo mshindi wa kwanza atajishindia gari jipya aina ya Range Rover sport inaendelea na watu wote wameombwa kushiriki bahati nasibu hiyo.
“Tunawaomba watu wote washiriki kwa kuandika neno SHINDA kwa kutumia simu zao za mkononi na kutuma kwa sms kwenda namba 15567 ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali na wakati huohuo wakichangia yatima wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”

Imeandaliwa na kusainiwa naRena Callist,
CHAIRMAN,MISS EAST AFRICA BEAUTY PAGEANT.

Wednesday, September 2, 2009

african-musicians-battle-it-out-for the 2009 MTV MUZIKI AWARD WITH ZAINAY na Shaa safari hii ni moja kati ya wasanii watakaotuwakilisha kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards, fuatilia maelezo haya ili kujua zaidi.
SINA UJAUZITO WA MARLAW ..... BESTA
msanii besta na marima laurance (marlaw) wamekana tetesi zinazoendelea kuwa wanauhusiano wa kimapenzi na kuwa besta anaujauzito wa msanii huyo.
nimeongea na besta na haya ndio aliyoyasema "sio kweli jamani mi sina ujauzito niko kawaida kabisa na marlaw mi ni rafiki yangu tu wa karibu, na wala sina mahusiano ya kimapenzi nae mi nna wangu nae anawake" amesema besta

wakati marlaw pia amekana tuhuma hizo na kusema "hizo habari nimeziskia mda tu lakini hazina ukweli, besta mi ni rafiki yangu saaaaaana na ni jirani yangu lakini sina uhusiano nae. natamani hata umuite sasa hivi uhakikishe kama ana mimba maana hii kuongea kwenye sim inaweza ikawa sio baadae mkaona kama kaitoa .
LABOUR DAY WEEKEND MJINI WASHNGTON DC
LABOR BAY WEEK END WASHINGTON DC
KAMPUNI YA DMK IKISHIRIKIANA NA DMV INTERNATIONAL COMMUNITY WANA WALETEA LABOR DAY WEEK END KAMA IFUATAVYO
**FRIDAY/ IJUMAA SEPT 4 - PARTY WITH THE BEST VIP STYLE- @ CLUB- OZIO V I P LOUNGE-1813 M ST,NW.DC, 4 FLOORS OF ENTERTAINMENT

**SATURDAY/J MOSI SEPT 5 - HII NDIO MAIN EVENT-LADIES FREE B4 12,FELLAS HALF OFF B4 12 @ CLUB- GALLERY LOUNGE S.SPRING DOWN TOWN-1115 EAST WEST HIGH WAY,S.SPRNG,MD

THE BEST DJS FROM 95.5WPGC,93.9WKYS,GUEST INTERNATIONAL DJS MATAIFA YOTE YATAKUWA HAPA-LABOR DAY MAYHEM INTERNATIONAL STYLE.

ALSO SURPRISE LIVE PERFORMANCE- HIS NEW SINGLE INAYOTAMBA B.E.T
**SUNDAY/COOLDOWN-SEP 6-BYE BYE SUMMER WATER MELON STYLE @ULTRA BAR DC,911 F STREET,NW,DC-DJ ARMAGEDON,DJMAMUSH

THIS SUNDAY PARTY WITH ETHIOPIAN,ERITREA,RWANDA,BURUNDI-YES WE GOT THIS

DMK STYLE JUST ASK SOMEBODY.MAELEZO- 301-661-6207 / 202-321-0184 / WEB* WWW.DMKPRODUCTION.COM
malighafi ya clouds tv ikiandaliwa

Wana wa Clouds Tv wakiwa mzigoni wakiandaa malighafi kwa ajili ya kwenda hewani siku chache zijazo.
jitokeze mbele za watu,uonekane wa tofauti na shear illussions daima

cheki mambo hayo

si ya kitoto alafu ushindwe kupendeza watakucheka wenzio
NGOMA YA MFALME MSWATI WA III KUCHAGUA MKE USWAZI

wasichana hucheza na kuimba huku wakitegemea kuteuliwa na Mfalme
Mfalme Mswati III katika ngoma hiyo jana huko Mbabane
Kaka Michuzi,
nipo huku Swaziland na jana na leo tulikuwa tunashuhudia ngoma yenye mvuto wa kipekee kwa jamii ya Waswazi ya Reed Dance, ni tukio ambalo ufanyika kila mwaka mara moja katika kipindi kama hiki.
Ngoma hii inawahusisha wasichana wenye umri kuanzia miaka mitano mpaka 25, kipindi ambacho King Mswati upata fursa ya kupata mke mwengine. Kwa sasa ni mwaka wa tatu hajachagua mke wa kuona kutoka katika utaraibu wa kumpata kupitia ngoma hii,!
Kwa kweli Waswazi wanatumia kipindi hiki kama sehemu ya kupata mapato ya utalii kwa nchi yao kwani watu wa mataifa mbalimbali wamekuja hasa jamaa zetu kutoka China ndio wengi, Muhimu ninalojifunza kuwa hawa Wachina pamoja na kuja kama watalii lakini wamekwisha pata dili za kufanya kutokana na ngoma hii. naleta picha hizi chache nilipiga jana na za leo nitawatumia baadaye
Mdau wa muda hapa Swaziland


WASICHANA BIKRA TOKA KILA PEMBE YA USWAZI HUJITOKEZA

NI NGOMA KUTWA NZIMA

FURAHA NA VICHEKO

all right reserved by makii.blogspot.com
Wavulana husindikiza dada zao

counters