Inakimbizaaaaa


Thursday, September 10, 2009

UNAWAJUA MAPACHA HAWA WAKO NDANI YA BBA 4


Shindano la nne la Big Brother limeanza jana jijini Johannesburg kwa mbwembwe za hali ya juu huku mabadiliko makubwa yakijitokeza kama kauli mbiu yao "mapinduzi" isemavyo.

Moja ya vivutio vikubwa katika uzinduzi wa shindano hilo ni pamoja na uhusishwaji wa mastaa wa tasnia ya filamu barani Afrika ambapo msanii Kanumba wa Tanzania aliungana na mastaa wengine watatu katika jumba hilo kuwakaribisha washiriki 11 kati ya washiriki 14 wanaotakiwa katika nyumba hiyo.
Moja ya mambo yaliyostua wadau na wapenzi wengi wa shindano hilo la Big Brother Revolution 2009 ni pamoja na kutoingia kwa washindani 3 wa nchi za Tanzania, Angola na Zambia kitendo kilichotafsiriwa na wengi ya kuwa huenda Kanumba ndiye mshiriki kamili wa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo meneja masoko wa kampuni ya Multi Choice Tanzania aliwataka watanzania kuwa na subira ili kujua hatma ya ushiriki wao.

Uzinduzi huo ambao uliongozwa na MC mahiri kabisa IK kutoka nchini Nigeria ilipambwa na burudani toka kwa K'naan na pia ilikuwa na surprise ya washiriki mapacha kutoka Namibia pamoja na washiriki mmoja mmoja zaidi kutoka Kenya na Uganda.
Aidha washiriki wote 12 walioingia ni wanaume na waliobaki inasemekana ni wanawake hivyo kuweka shauku ya hali ya juu kwa watazamaji wa shindano hilo.

No comments:


counters