Ambwene Yesaya (ay)
habari zimeingia punde zinadatisha kwamba mwanamuziki nyota wa kizazi kipya ambwene yesaya a.k.a AY anaondoka Jumamosi hii kuelekea sauzi katika jiji la johannesburg ambako atatumbuiza kwenye hafla ya Big Brother. Ataongozana na Snare wa east coast.
AY kaiambia globu ya jamii kwa njia ya twitter sasa hivi kwamba yeye kama kawaida yake hana show kubwa wala ndogo na kwamba show zote kwake ni muhimu hivyo anajiandaa kwa makamuzi ya nguvu.
kasema baada ya sauzi ataelekea Malaysia ambako atakuwa na show jijini Kuala lumpur September 24, mwaka huu ndani ya klabu cha Titunium. Pia ataporejea wiki ijayo anatarajiwa kutoa singo ingine mpya iitwayo 'Bed & Breakfast' ambayo imetayarishwa na Hermy B wa B. Hitz Studios.
Wakati huo huo AY anawakumbusha wadau wote popote walipo hapa bongo kumpa taffu kwa kumpigia kura katika tuzo za Mtv Africa. Kumpigia kura andika 'BHH AY' kisha tuma sms kwenda namba 0789 777 333
No comments:
Post a Comment