Ilikuwa ‘lokesheni’ katika moja ya nyumba maarufu za ‘shuuting’ huko Mbezi-Beach, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo Wema alibambwa na Kamera ya Ijumaa akiwa na donda katika goti la mguu wake wa kulia.
Baada ya kuona jereha hilo, king’ora cha ubongo wa Paparazi Wetu kilianza kugonga kutaka kujua kulikoni.
Mbali na kidonda, upekuzi wa ‘bodi’ la mnyange huyo anayeongoza kwa kufanya vichwa vya habari za mastaa ‘town’, ulionesha baadhi ya maeneo ya mwili wake yakiwa ‘full’ mistari miekundu na hivyo kupoteza mvuto uleee!
Ilibidi kuanza kuhoji kilichosababisha mrembo huyo kuharibika ngozi yake nyororo, ambapo katika nusanusa ya hapa na pale, mmoja wa mastaa wenzake ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, alilinong’oneza Ijumaa kwamba, mabadiliko ya ngozi ni jambo la kawaida linaloweza kuwatokea baadhi ya wanawake lakini hustawi zaidi baada ya matumizi ‘tuumachi’ ya vipodozi.
CHEKI MIGUU YAKE ILIVYO
“Mabadiliko ya ngozi hasa kuwa na michirizi na wakati mwingine mistari, siyo ishu kubwa kwa baadhi ya wanawake, lakini inaweza kuwa ishu endapo vipodozi hivyo vitakuwa too much,” alisema staa huyo aliyekiri kuwa, hata yeye alishangaa alipomwona Wema akiwa na michirizi kibao mwilini.
Ilibidi Ijumaa liongee na mtaalamu wake wa masuala ya afya ya ngozi ambaye alibainisha kwamba, kupasuka kwa ngozi na kuwa na mistari miekundu (scrabs) kwa wanawake kunaweza kusababishwa na mambo makuu mawili.
Mtaalamu huyo aliyataja mambo hayo kuwa ni unene na matumizi ya vipodozi kama vile ‘carolight’ yenye kemikali za ‘hydroquine’ zinazosababisha madhara makubwa kwa ngozi ya binadamu.
Alisema kwa mwanamke ambaye si mnene lakini akatoka michirizi hiyo, mara nyingi ni matumizi ya vipodozi vyenye kemikali.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumsaka Wema kupitia kilongalonga chake ili aeleze kidonda hicho kilisababishwa na nini, hakuweza kupatikana.
No comments:
Post a Comment