Inakimbizaaaaa


Wednesday, September 2, 2009

NGOMA YA MFALME MSWATI WA III KUCHAGUA MKE USWAZI

wasichana hucheza na kuimba huku wakitegemea kuteuliwa na Mfalme
Mfalme Mswati III katika ngoma hiyo jana huko Mbabane
Kaka Michuzi,
nipo huku Swaziland na jana na leo tulikuwa tunashuhudia ngoma yenye mvuto wa kipekee kwa jamii ya Waswazi ya Reed Dance, ni tukio ambalo ufanyika kila mwaka mara moja katika kipindi kama hiki.
Ngoma hii inawahusisha wasichana wenye umri kuanzia miaka mitano mpaka 25, kipindi ambacho King Mswati upata fursa ya kupata mke mwengine. Kwa sasa ni mwaka wa tatu hajachagua mke wa kuona kutoka katika utaraibu wa kumpata kupitia ngoma hii,!
Kwa kweli Waswazi wanatumia kipindi hiki kama sehemu ya kupata mapato ya utalii kwa nchi yao kwani watu wa mataifa mbalimbali wamekuja hasa jamaa zetu kutoka China ndio wengi, Muhimu ninalojifunza kuwa hawa Wachina pamoja na kuja kama watalii lakini wamekwisha pata dili za kufanya kutokana na ngoma hii. naleta picha hizi chache nilipiga jana na za leo nitawatumia baadaye
Mdau wa muda hapa Swaziland


WASICHANA BIKRA TOKA KILA PEMBE YA USWAZI HUJITOKEZA

NI NGOMA KUTWA NZIMA

FURAHA NA VICHEKO

all right reserved by makii.blogspot.com
Wavulana husindikiza dada zao

No comments:


counters