Inakimbizaaaaa


Monday, August 31, 2009

BENKI KUU YACHAPISHA NOTI MPYA YA SH 2,000 YALE YALE YA ZIMBABWE

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa noti mpya za Sh2,000 ambazo zitatumika sanjari na zilizopo kwenye mzunguko kwa sasa.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba, lengo la kutoa noti hizo mpya ni kukidhi mahitaji yake kwenye mzunguko wa fedha nchini.

"Noti hizi mpya zinatofauti moja tu na zile ambazo zimo kwenye mzunguko kwa sasa nayo ni saini zilizopo.

Saini zilizopo kwenye noti mpya ni za Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,” alisema.

Friday, August 28, 2009

NATAMANI KUWA MALAIKA LADY JAY DEE
lady jay dee amechia wimbo mpya ambao video yake ndio hii inaitwa NATAMANI KUWA MALAIKA.

Friday, August 21, 2009

POWER BREAKFAST YAWAPA BURUDANI YA KUKATA NA SHOKA WADAU

Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL sasa ameanza kushika Camera ya Video, naona labda anafanya mazoezi kabla ya Kituo cha televisheni cha mjengoni hakijaanza ili aweze kukamata Dimba la kupiga Picha hongera kaka hapa anaonekanaakimuelekeza kitu mtangazaji mwenzie Rommy J. hapo mjengoni wa kipindi cha The Blog


Waigizaji maarufu nchini Kanumba na Aunt wakifanya vibweka mbele ya Camera ya Kamanda mshika Camera wa FULLSHANGWE hebu wacheki mdau.

Hapa ni Pipi mwanamuziki wa THT,P. Funk Producer maarufu nchini Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchmark Production na mwandaaji wa Bongo Star Search na mwanamuziki Sara wakipozi kwa picha.

Mdau wa siku nyingi katika muziki ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa mwanamuziki Mr II kutoka Marekani Nurueli kati, Sara wanablog wa angaliabonngo.blogspot.com kul;ia na mdau Lugano

Hapa Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Juhayna Kusaga akipata shangwe za Blue3 na marafiki zake wakati kundi hilo lilipokuwa likifanya mambo yake jukwaani.


Nyota wetu wa kikapu Hasheem Thabeet katikati ambaye anacheza mpira wa kikapu nchini Marekani na marafiki zake hawakuwa nyuma kupata burudani wakati wa tafrija ya kujipongeza ya kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi na Redio Clouds ya jijini.


Watangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi Gerald Hando na Babra Hassan wakiongea kwa kuigiza mbele ya wageni waalikwa kama wanavyotangaza redioni, wakati wa tafrija ya kujipongeza iliyoandaliwa mahsusi kwa wadau mbalimbali wa kipindi hicho ilifanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick jijini ambapo kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa kundi la Blue3 kutoka Uganda, Marlow na wasanii wa kundi matata la THT kutoka jijini, hebu mdau ambaye hukuwepo pata matukio katika picha ili kujua wadau waliojimuvuzisha na kuvinjari katika Tafrija hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka sisi FULLSHANGWE kama kawaida yetu tulipenya na kuingia humo na mambo yalikuwa Mujaraarabu kabisa.
Tabasamu imening’arisha.!

Baadhi ya mashabiki na wapenzi wake wanamtambua kwa jina la Steve r&b,lakini jina lake la kuzaliwa anaitwa Stephen William,mtoto wa pili katika familia ya mzee Stephen.

Mwenyewe anakiri wazi kuwa nyota yake ilianza kung’ara pale aliposhirikishwa ndani ya wimbo wa Tabasamu ulioimbwa na Mr Blue,ambao kusema kweli alionekana kufanya vyema na kupelekea kukubalika kwa haraka mbele ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Steve anasema kufuatia kukubalika huko,kumempelekea aonyeshe kipaji chake zaidi cha kuimba,na ndipo akaibuka na singo yake ya kwanza iliyojulika kwa jina la nimeshindwa,kama vile haitoshi akatoka tena na wimbo wake ulioitwa nisamehe na sasa anatamba na wimbo wake mwingine uitwao sogea karibu.

Baada ya kutoa singo hizo tatu,Steve ambaye kwa sasa yupo chini ya kampuni ya Zizzou Entertainment inayomilikiwa na mmoja wa wafanyabiashara mahiri hapa Bongo,Athuman Tippo,tayari amekwisha ikamilisha albamu yake ya kwanza yenye jumla ya nyimbo kumi,ambayo mpaka sasa bado hajaipa jina.

“Nyimbo zote nimezirekodia katika studio mbalimbali ikiwemo Combinations Souns prodyuza akiwa ni Man Walter,Eagiez Records produza akiwa ni Nice P,Kiri Records pamoja na GA Music, hivyo washabiki wa bongofleva wakae mkao wa kula kwani nakuja kwa spiidi ya r&B”.
PPF PLAZA MWANZA

baada ya kukamilika awamu ya kwanza (shoto) PPF Plaza inaendelea na ujenzi ambapo upande huu wa kulia kutakuwa na hoteli kubwa ya kitalii ya nyota tano. Rock City inaendelea kuwa mswano kwani kutakuwa na hoteli mbili zenye hadhi ya kimataifa
PREMIERE OF FILM 'CONFUSION IN ROCK CITY' Saturday 22nd August,2009 @nyumbani Hotel in Mwanza.
SALAMA JABIR & GADNER G HABASH TAKE OVER MWANZA WITH ‘CONFUSION IN ROCK CITY”
This Saturday, August 22, 2009, all roads lead to Mwanza. ZM productions, with sponsorship from Air Tanzania Company Limited and Nyumbani Hotel & resorts will unveil the up and coming film ‘Confusion in Rock City’ to the selected few of Mwanza.

MKE WA RAISI WA MAREKANI ALIPOACHA GUMZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KWA KUVALIA KIKAPUTULA

Vyombo vingi vya habari vya Marekani vimekuwa vikijadili nguo anazovaa Michelle Obama kama zinafaa kuvaliwa na mke wa rais au la huku watu wengine wakitoa maoni kwamba Michelle ni mwanamke kama wanawake wengine hivyo ana haki ya kuvaa atakavyo.
Mdau KB.

KIKAPUTULA KINAPOTINGA IKULU
Mkuu wa Wilaya ya Nanihii,
Mke wa rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama amezidi kuonyesha tofauti yake na wake wa marais waliopita wa Marekani. Michelle amekuwa mke wa kwanza wa rais kuvaa kikaptula na kupanda dege la rais Air Force One.



Obama, mkewe na binti zake walikuwa Arizona katika vakesheni yao binafsi ya kutembelea sehemu mbali mbali za kitalii katika jimbo hilo lakini vyombo vya habari badala ya kushughulika na ziara ya mkuu huyo wa taifa kubwa duniani, walikuwa bize kupata taswira za kikaptula cha mke wa rais.

counters