Inakimbizaaaaa


Friday, August 21, 2009

Tabasamu imening’arisha.!

Baadhi ya mashabiki na wapenzi wake wanamtambua kwa jina la Steve r&b,lakini jina lake la kuzaliwa anaitwa Stephen William,mtoto wa pili katika familia ya mzee Stephen.

Mwenyewe anakiri wazi kuwa nyota yake ilianza kung’ara pale aliposhirikishwa ndani ya wimbo wa Tabasamu ulioimbwa na Mr Blue,ambao kusema kweli alionekana kufanya vyema na kupelekea kukubalika kwa haraka mbele ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Steve anasema kufuatia kukubalika huko,kumempelekea aonyeshe kipaji chake zaidi cha kuimba,na ndipo akaibuka na singo yake ya kwanza iliyojulika kwa jina la nimeshindwa,kama vile haitoshi akatoka tena na wimbo wake ulioitwa nisamehe na sasa anatamba na wimbo wake mwingine uitwao sogea karibu.

Baada ya kutoa singo hizo tatu,Steve ambaye kwa sasa yupo chini ya kampuni ya Zizzou Entertainment inayomilikiwa na mmoja wa wafanyabiashara mahiri hapa Bongo,Athuman Tippo,tayari amekwisha ikamilisha albamu yake ya kwanza yenye jumla ya nyimbo kumi,ambayo mpaka sasa bado hajaipa jina.

“Nyimbo zote nimezirekodia katika studio mbalimbali ikiwemo Combinations Souns prodyuza akiwa ni Man Walter,Eagiez Records produza akiwa ni Nice P,Kiri Records pamoja na GA Music, hivyo washabiki wa bongofleva wakae mkao wa kula kwani nakuja kwa spiidi ya r&B”.

No comments:


counters