Hapa ni Pipi mwanamuziki wa THT,P. Funk Producer maarufu nchini Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchmark Production na mwandaaji wa Bongo Star Search na mwanamuziki Sara wakipozi kwa picha.
Mdau wa siku nyingi katika muziki ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa mwanamuziki Mr II kutoka Marekani Nurueli kati, Sara wanablog wa angaliabonngo.blogspot.com kul;ia na mdau Lugano
Hapa Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Juhayna Kusaga akipata shangwe za Blue3 na marafiki zake wakati kundi hilo lilipokuwa likifanya mambo yake jukwaani.
Nyota wetu wa kikapu Hasheem Thabeet katikati ambaye anacheza mpira wa kikapu nchini Marekani na marafiki zake hawakuwa nyuma kupata burudani wakati wa tafrija ya kujipongeza ya kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi na Redio Clouds ya jijini.
Watangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi Gerald Hando na Babra Hassan wakiongea kwa kuigiza mbele ya wageni waalikwa kama wanavyotangaza redioni, wakati wa tafrija ya kujipongeza iliyoandaliwa mahsusi kwa wadau mbalimbali wa kipindi hicho ilifanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick jijini ambapo kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa kundi la Blue3 kutoka Uganda, Marlow na wasanii wa kundi matata la THT kutoka jijini, hebu mdau ambaye hukuwepo pata matukio katika picha ili kujua wadau waliojimuvuzisha na kuvinjari katika Tafrija hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka sisi FULLSHANGWE kama kawaida yetu tulipenya na kuingia humo na mambo yalikuwa Mujaraarabu kabisa.
No comments:
Post a Comment