Inakimbizaaaaa


Friday, November 6, 2009

TAMASHA LA FIESTA ONE LOVE LASOGEZWA MBELE


Tamasha la Fiesta One Love 2009 lililotarajiwa kufanyika jumamosi hii,Novemba 7 katika uwanja wa posta,kijitonyama jijini Dar,limeaihirishwa na kusogezwa mbele.

Akizungumza mratibu mkuu wa tamasha hilo Bw.Ruge Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo limeaihirishwa hadi Novemba 21,mabadiliko hayo yanatokana na wahusika wakuu wakiwemo wafanyakazi wa Clouds Media Group/Prime Time Promotions (ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo waandaji wa tamasha hilo) kuondokewa (kufariki) kwa Mwenyekiti wao Mzee Alex Mkama Kusaga juzi jioni nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu.

Mutahaba amesema ratiba ya wasanii wambao walipaswa kushiriki kwenye tamasha hilo la Kitaifa iko pale pale wala haijabadilika,na kwamba msanii ambaye alitajwa angewatumbuiza wakazi wa Dar kutoka chini Marekani kwenye tamasha hilo,Buster Rhymes na wenzake naye ratiba yake iko pale pale,kwamba atakamua vilivyo siku hiyo. .
Aidha kwa taarifa za msiba wa Mzee K. inaelezwa kuwa mwili wake utawasili leo jioni na msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na Girrafe Hotel,kuhusu ratiba za mazishi na mambo mengine tutaendelea kufahamishana zaidi.

Wednesday, November 4, 2009

MPIGIE KURA ELIZABETH AWEZE KUBAKI BIGBROTHER AFRICA 4


KILA Mtanzania popote alipo ampigie kura Mtanzania mwenzetu na mdogo wetu ELIZABETH GUPTA asitoke kwenye Big Brother week hii.
Nitashukukuru sanaNaomba kila unapoingia kwenye mtandao u-log In kwenye tovuti ya www.mnetafrica.com/bigbrother na register yourself to VOTE for our youngest sister ELIZABETH GUPTA. Kujisajili ni rahisi kabisa piga kura kila baada ya saa moja tumwezeshe ELIZABETH mdogo wetu na Mtanzania mwenzetu asitoke kwenye Big Brother week hii na na kumbuka kura yako ndiyo itamwezesha kujishindia kitita cha $200,000 kila kitu kinawezekana ila kwa kura yako tuu! Naomba uwatumie rafiki zako wote ujumbe huu wamwezeshe MDOGO WETU ELIZABETH GUPTA apite.Ukitaka kupiga kura click kwenye neno VOTE na hapo utafuata utaratibu.Nakushukuru sana kwa ushirikiano wako.

EVELYNE ASHINDA TUZO YA MISS NATIONAL CUSTOMER

Mshindi wa pili wa Miss Universe Tanzania Evelyne Amasi ambaye anashikilia taji la Miss Earth Tanzania 2009, ameshinda tuzo ya Miss National Costume.

Mashindano ya Miss Earth ambayo yanafanyika tangu Novemba mosi mpaka 22 mwaka huu, huko nchini Philippines, Evelyne Amasi (23), mrembo ambaye ameondoka nchini mwishoni mwa mwezi wa kumi kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kumtafuta Miss Earth, ameshinda tuzo ya vazi la taifa (National costume) katika mashindano ambayo yalishirikisha zaidi ya warembo 80 kutoka nchi mbali mbali duniani kote.

Evelyne ambaye aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi huu( Oktoba 31), alifanikiwa kushinda tuzo ya Miss National Costume 2009 na kutwaa nishani na pesa taslimu ambayo atakuja kupewa siku ya fainali.

Ushindi wa Mrembo huyu, ulikubaliwa na wengi kutokana na uzuri na uasili wa mavazi ya mrembo huyu.

Mavazi ya mwanadada huyu yalikuwa tofauti na mavazi ya warembo wengine kwani zilikuwa zimetengenezwa kwa kutumia kambakamba zilizotokana na magome ya miti ambazo zimesukwa kwa ustadi na kuwakilisha vyema matumizi halisi ya mazingira yetu.

Mbali ya vazi hilo ambalo lilionekana kama kichaka cha mti vilevile kulikuwa na nyoka aliyetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu na juu kichwani kulikuwa na kilemba ambacho kimetumika kama kichaka cha ndege anachotagia mayai yake. Nguo hiyo ilibuniwa na mbunifu chipkizi Diana Magese toka mkoani Morogoro.

Katika kinyanganyiro hicho Evelyne ndio alikuwa mshindi wa kwanza kushinda tuzo hiyo akifuatiwa na mrembo toka Puerto Rico na Miss Guam.Katika mashindano haya, washindi wanaofanikiwa kushinda tuzo ndogondogo ndio wenye nafasi kubwa ya kuingia nusu fainali yaani top Sixteen(16 bora)Mwaka jana Tanzania iliwakilishwa na mrembo Miriam Odemba na kufanikiwa kuitangaza vyema nchi yetu kwa kuingia katika kumi na tano bora ya mavazi ya ufukweni na vazi la Taifa katika mashindano madogo na hatimaye kushika nafasi ya pili katika fainali na kutwaa taji la Miss Earth Air-2008, ambapo mshindi wa kwanza alitoka nchini Phillipines.Fainali za mashindano ya Miss Earth mwaka huu yatafanyika tarehe 22 mwezi wa kumi na moja huko Boracay Island nchini Philippines.

Jk akutana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini, aagana na balozi wa algeria leo ikulu

JK akiagana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Bwana Alberic Kacou muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar leo
Balozi wa Algeria nchini Tanzania anayemaliza muda wake Abdelmoun 'aam Ahriz akimwonesha JK majarida mbalimbali wakati balozi huyo alipokwenda ikulu kumuaga JK leo

ZAWADI YA MILLIONI KUMI WAREMBO WA MISS ILALA WAPAGAWA DAR WEST PARK INN -TABATA


Kivumbi cha kumpata mrembo wa Fainali za Miss Utalii Ilala 2009 ni tarehe 6/11/2009 Ijumaa katika ukumbi wa Da’ West Park Inn Tabata, ambapo jumla ya Warembo 12 watapanda katika jukwaa kuchuana kuwania taji kwa msimu wa 2009/2010.

Katika shindano hilo ambalo macho na masikio kwa wakazi wa Dar es Salaam limewatia wazimu kutokana na kutoelewa nani hataibua nderemo, Vifijo, na makelele kutokana na warembo wote kuwa katika hali ya Ushindani mkali ambapo kila mrembo amejigamba kuibuka na taji hilo kasha kubeba vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha thamani yake ikiwa ni milioni mbili .

Warembo hao walioanza kambi kwa takribani mwezi mmoja katika Ukumbi wa Da’ West Park Inn-Tabata, waliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii unaopatikana Tanzania ikiwemo Hifadhi za Utalii za Taifa, Vivutio vya Kitalii, pamoja na Maajabu ya Dunia yanayopatikana hapa Tanzania.

Aidha katika shindano hilo, warembo hao wataonyesha Mavazi ya asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania, watacheza ngoma kuonyesha utamaduni wa Mtanzania, Watavaa mavazi ya Kitanzania ya Kitalii, vazi la Ubunifu lililotengenezwa kwa maligafi za hapa Tanzania, pamoja na mengine mengi yanayohusiana na masuala ya Utamaduni wa Mtanzania.

Warembo wanaowania taji la Miss Utalii Ilala 2009 ni pamoja na ,Tickey Lighton,Neema King’aka, Edna Endrew, Frola Nicholaus, Sheila Baamary, Janeth Samson, Nezia Gabriel, Roselina Sekwao, Jamida Abdu, Aghata Kilala, Tabus Thomas, na Shaymin Ntemena. Zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni kumi zitatolewa kwa washindi na washiriki, ikiwa ni pamoja na Fedha, na vifaa mbalimbali vyenye thamani mbalimbali, zitalolewa kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza kwa mujibu wa Waandaji wa shindano hilo ni thamani ya shilingi milioni 2, mshindi wa pili thamani ya million moja na laki mbili ,mshindi wa tatu thamani ya laki nane na , mshindi wa nne na tano, thamani ya laki tano na mshindi wa Kipaji (Talent) ni thamani ya laki saba na nusu na kifuta jasho kwa wote ni shilingi elfu thelathini na watapatiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki moja kila mmoja.

Tuesday, November 3, 2009

KUMBE HATA MTONI KUNA (MENDE)

MISS TANZANIA AKABIDHIWA NDINGA YAKE

Miriam Gerald akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC1 Evance Mhando mara baada ya kukabidhiwa gari lake mchana huu.
Meneja anaehusika na magari wa Vodacom Tanzania(kulia) akimuelezea Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald wa pili toka kulia namna ya kutumia funguo za gari lake,wanaoshudia ni Meneja udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna,Mkuu wa itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoe.


Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwapungia waandishi wa habari ndani ya gari lake alilokabidhiwa na Vodacom Tanzania na shivacom lenye thamani ya shilingi Milioni 53


ndinga la vodacom miss tz 2009
Miriam Gerald kutoka Mwanza,alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.

Pamoja na kuzawadiwa mchuma wake,Miriam ataagwa keshokutwa kwenye kituo cha Uwekezaji,TIC kwa ajili ya safari yake ya jijin London Uingrereza na baadaye Afrika Kusini.
Miriam anatarajia kuondoka nchini ijumaa amabapo atashiriki mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa biashara ambao utaanza Novemba 9 hadi 11 nchini humo.

akizungumza hivi karibuni jijini Dar,Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa wanatarajia mrembo huyo atakwenda kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Lundenga alisema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Mkurugenzi wa TIC,Emmanuel Ole Naiko.

Mashindano ya MIss World 2009,yamepangwa kufanyika desemba 12,Sandton Convention Center,mjini Johannesburg.

Mashindano yataanzia London,ambako warembo watawasili Novemba 7,na Novemba 10,watakwenda Dubai,Falme za kiarabu,ambako wataunganisha ndege Novemba 15 kwenda Johannesburg.
Kombe la dunia
Ramani ya ziara kamili ya kombe hilo
Ndege aina ya Boeing 737 inayosafirisha kombe hilo
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kuwa ziara ya Kombe la Dunia kwa nchi za Afrika inaendelea vizuri na kwamba hakuna matatizo yoyote yaliyotokea tangu kuzinduliwa kwake nchini Uswiss na kuanza ziara katika bara hilo nchini Misri...

NANI KUIBUKA NA MCHUMA JUMAMOSI HII KWENYE FIESTA ONE LOVE


Huu ndiyo mchuma wenyewe utakaowaniwa siku ya jumamosi kwa yoyote atakayebahatika,kikubwa ni kuinunua tiketi yako ya Fiesta one love mapema kabisa na bahati nasibu itachezeshwa siku ya jumamosi saa moja usiku,kwa hiyo ni vyema ukawahi unaweza kubahatika na kuibuka na huo mchuma halafu mambo yakwa swafiii kabisa.Tiketi ni 10,000/= ukiwahi mapema,ukichelewa 15,000/=.Changamka

LIBENEKE LA MOHAMED DEWJI

Mbunge wa Singida Mh. Mohamed Dewji akisakata ngoma na bendi ya Twanga Pepeta iliyokuwa inatumbuiza uwanja wa Namfua Singida karibuni. picha na habari zaidi nenda kwenye libeneke lake kama ilivyooneshwa hapo chini

Kaka Msacky,
Ninakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya ya kutupasha habari mbalimbali za kijamii. Ningependa kuwaomba wadau mtupe ushirikiano wa kutoa mawazo na pia kuitembelea blog yetu ya Mhe. Mohammed Dewji "Mo", ambapo tutakuwa tunapeana habari mbalimbali na pia kujadili masuala mbalimbali yanayohusu jamii yetu ya kitanzania.
Blog hii ni changa lakini ninaamini tutafika mbali kwa msaada na ushirikiano kutoka kwa wadau. Vile Vile Mo atatumia uwanja huu kujadiliana na wadau jinsi ya kuboresha na kuleta maendeleo ndani ya jamii

tovuti yetu ni
http://www.mohammeddewji.com/
na blog yetu ni
www.mohammeddewji.com/blog
Globu ya Jamii inampongeza Mh. Mohamed Dewji kwa uamuzi wa kuanzisha libeneke, ikiwa ni njia mojawapo ya kupasha na kupata habari kwa njia ya kisasa ambayo ni ya haraka na isiyongoja kesho. mambo ni papo kwa papo. Natumai Wah. wengine, ambao bila shaka wana kigugumizi endapo kama kuna haja ya kuanzisha libeneke ama la, wataiga mfano huu. Hongera Mo.

counters