Mashindano ya Miss Earth ambayo yanafanyika tangu Novemba mosi mpaka 22 mwaka huu, huko nchini Philippines, Evelyne Amasi (23), mrembo ambaye ameondoka nchini mwishoni mwa mwezi wa kumi kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kumtafuta Miss Earth, ameshinda tuzo ya vazi la taifa (National costume) katika mashindano ambayo yalishirikisha zaidi ya warembo 80 kutoka nchi mbali mbali duniani kote.
Evelyne ambaye aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi huu( Oktoba 31), alifanikiwa kushinda tuzo ya Miss National Costume 2009 na kutwaa nishani na pesa taslimu ambayo atakuja kupewa siku ya fainali.
Ushindi wa Mrembo huyu, ulikubaliwa na wengi kutokana na uzuri na uasili wa mavazi ya mrembo huyu.
Mavazi ya mwanadada huyu yalikuwa tofauti na mavazi ya warembo wengine kwani zilikuwa zimetengenezwa kwa kutumia kambakamba zilizotokana na magome ya miti ambazo zimesukwa kwa ustadi na kuwakilisha vyema matumizi halisi ya mazingira yetu.
Mbali ya vazi hilo ambalo lilionekana kama kichaka cha mti vilevile kulikuwa na nyoka aliyetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu na juu kichwani kulikuwa na kilemba ambacho kimetumika kama kichaka cha ndege anachotagia mayai yake. Nguo hiyo ilibuniwa na mbunifu chipkizi Diana Magese toka mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment