Meneja anaehusika na magari wa Vodacom Tanzania(kulia) akimuelezea Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald wa pili toka kulia namna ya kutumia funguo za gari lake,wanaoshudia ni Meneja udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna,Mkuu wa itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoe.
Miriam Gerald kutoka Mwanza,alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga. Pamoja na kuzawadiwa mchuma wake,Miriam ataagwa keshokutwa kwenye kituo cha Uwekezaji,TIC kwa ajili ya safari yake ya jijin London Uingrereza na baadaye Afrika Kusini.
Miriam anatarajia kuondoka nchini ijumaa amabapo atashiriki mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa biashara ambao utaanza Novemba 9 hadi 11 nchini humo.
akizungumza hivi karibuni jijini Dar,Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa wanatarajia mrembo huyo atakwenda kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Lundenga alisema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Mkurugenzi wa TIC,Emmanuel Ole Naiko.
Mashindano ya MIss World 2009,yamepangwa kufanyika desemba 12,Sandton Convention Center,mjini Johannesburg.
Mashindano yataanzia London,ambako warembo watawasili Novemba 7,na Novemba 10,watakwenda Dubai,Falme za kiarabu,ambako wataunganisha ndege Novemba 15 kwenda Johannesburg.
No comments:
Post a Comment