Mbunge wa Singida Mh. Mohamed Dewji akisakata ngoma na bendi ya Twanga Pepeta iliyokuwa inatumbuiza uwanja wa Namfua Singida karibuni. picha na habari zaidi nenda kwenye libeneke lake kama ilivyooneshwa hapo chini
Kaka Msacky,
Ninakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya ya kutupasha habari mbalimbali za kijamii. Ningependa kuwaomba wadau mtupe ushirikiano wa kutoa mawazo na pia kuitembelea blog yetu ya Mhe. Mohammed Dewji "Mo", ambapo tutakuwa tunapeana habari mbalimbali na pia kujadili masuala mbalimbali yanayohusu jamii yetu ya kitanzania.
Blog hii ni changa lakini ninaamini tutafika mbali kwa msaada na ushirikiano kutoka kwa wadau. Vile Vile Mo atatumia uwanja huu kujadiliana na wadau jinsi ya kuboresha na kuleta maendeleo ndani ya jamii
tovuti yetu ni
http://www.mohammeddewji.com/
na blog yetu ni
www.mohammeddewji.com/blog
Globu ya Jamii inampongeza Mh. Mohamed Dewji kwa uamuzi wa kuanzisha libeneke, ikiwa ni njia mojawapo ya kupasha na kupata habari kwa njia ya kisasa ambayo ni ya haraka na isiyongoja kesho. mambo ni papo kwa papo. Natumai Wah. wengine, ambao bila shaka wana kigugumizi endapo kama kuna haja ya kuanzisha libeneke ama la, wataiga mfano huu. Hongera Mo.
No comments:
Post a Comment