Inakimbizaaaaa


Friday, September 25, 2009

DIBANJI KUTUA DAR KWA AJILI YA MTV AFRICA MUSIC AWARDS


Msanii D'Banj kutoka Nigeria ambae anatamba na wimbo wake Fallin Love, anakuja Dar es Salaam tar 3 October kwa ajili ya show na baadae ataelekea Nairobi kwa ajili ya uwepo wake katika tuzo za MTV...
Kwa mengi zaidi tembelea mtvbase.com na pages mbali mbali za MTV kama facebook na twitter
Kutoka kwetu Tanzania tutawakilishwa na AY na SHAA

Thursday, September 24, 2009

WAANDAAJI WA MAISHA PLUS WAKUMBWA NA TUHUMA YA KUPOKEA HONGO


waandaaji wa kipindi cha televishen kinachojulikana kama maisha plus wamekumbwa na tuhuma ya kupokea hongo kutoka kwa mshindi wa kipindi hicho. kutokana na gazeti la DAILY NEWS waandaaji hao walimtaka mshindi kuwapatia milioni 3 katika milioni 10 aliyoshinda. Mmoja wa waandaaji hao masood kipanya amesema tuhuma hizo hazina maana yoyote na sishangai kuskia hili hasa wakati huu ambapo maisha plus ndio inaongezeka umaarufu.tuhuma hizi zinatoka kwa maadui tu ambao wanataka kuniharibia sifa yangu amesema kipanya.lakini wameendela kusema kuwa waandaaji hao waitoa offa hiyo kwa washiriki wengine lakini walikataa.mshindi wa maisha plus mwaka huu anatarajiwa kupata shilingi million 15 tofauti na mwakajana.

Wednesday, September 23, 2009

AY APOKELEWA KWA PART MALYASIA







Hizi ni Picha maalum za welcome Party aliyofanyiwa jana msanii AY kwenye Club ya HELO BALI mjini Kualar Lumpa, Malaysia. Show kamili inafanyika kesho tarehe 24 kwenye ukumbi wa TITUNIUM CLUB. Wabongo waishiyo Malaysia kazi kwenu kuona vitu vya 'nominee' wa MTV Africa Music Awards 2009!!!

HUYU NDIYE IRENE UWOYA WA UKWELI CHEKI MTOTO ALIVYOSIMAMA



Miss TZ & Talent show night ijumaa hii giraffe ocean view hotel


Warembo wa Miss TZ wakiwa katia uzi wa kutangaza utalii. Ijumaa September 25, 2009 watakuwa na Miss Tanzania Day & Talent Show night ambapo wadau wanakaribishwa Giraffe Ocean View hotel iliyopo Kunduchi kushuhudia warembo wakichuana katika shindano la vipaji mbalimbali walivyojaaliwa navyo kuanzia saa moja jioni. kiingilio ni alfu 40 kwa kichwa na mshindi wa shindano hilo atabeba laki 5 keshi.

Wednesday, September 16, 2009

UNAMFAHAMU LOVENESS LOVE (DIVA) WA CLOUDS FM ALA ZA ROHO SEASON 2

I can't believe the season Two of Keeping Up with the Diva is here already! It feels like the show just started!
Time flies so fast! The season is pretty intense. there is a lot of relationship drama in it this time via Clouds Fm Ala za Roho show witcha Diva Loveness Love.. Kuanzia nne kamili mpaka 6 kamili za usiku.. Everyday Jumatatu Mpaka Alhamis

http://www.diva255.com/

VIGGOGO WANNE WA BENKI KUU WAFIKISHWA MAHAKAMANI

VIGOGO wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 104 bilioni.

Vigogo hao ambao wote ni wakurugenzi wa BoT wa vitengo tofauti, walifikishwa mahakamani hapo asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Wameshtakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

Wakurugenzi hao wanashtakiwa kwa makosa tofauti ikiwamo kosa la tatu linalowahusisha wote wanne ambao ni Mkurugenzi wa Benki ya BoT, Simon Eliezer Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Kisima Thobias Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bosco Ndimbo Kimela na Mkurugenzi wa benki, Ally Farijallah Bakari.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincon alimwambia hakimu Samuel Maweda kuwa vigogo hao wanne, wakiwa watumishi wa umma walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kuisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146.

“Kwa pamoja na kwa makusudi walishindwa kuchukua tahadhari au kusahau majukumu yao katika mazingira nyeti, kwa udanganyifu walitayarisha nyongeza kwenye mkataba wa 2001 unaohusiana na uchapaji wa noti za benki kwa gharama kubwa ambapo bei ya mkataba huo iliisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146,” alidai Licon.

Licon aliendelea kuieleza mahakama kuwa mwaka 2004 washtakiwa Jengo na Mkango wakiwa ndani ya jiji na Mkoa wa Dar es Salaam na wakiwa wameajiriwa katika utumishi wa umma katika nyadhifa tofauti ndani ya BoT, kwa pamoja na kwa makusudi, wakiwa na lengo la kuvunja kanuni walitangulia kutoa ofa kwa wasambazaji wa noti za benki.Pauline Richard na Salim Said

Monday, September 14, 2009

INASADIKIKA KUWA MPAKANJIA AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa mume wa marehemu Amina Chifupa,Mohamed Mpakanjia amefariki leo mnamo majira ya saa tisa ,jioni hii katika hospitali ya jeshi ya Lugalo,Inaelezwa kuwa Mpakanjia alikuwa amelazwa hospitalini hapo toka juzi akisumbuliwa na ugonjwa wa Neumonia.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN

HUYU NDIE RAY BWANA (FATAKI) MZEE WA ATM...... ALL STAR

Wandugu nawatangulizia movie nyingine hiyo ambayo iko jikoni inapikwa "Fair Decision" itatoka soon baada ya "Divorce" ambayo itakuwa madukani kuanzia tarehe 29/9/2009. sina mengi saana itakapotoka pata nakala yako. Mdau Ray.
kwa picha na habari kibao
za tasnia ya filamu bongo

counters