Inakimbizaaaaa


Monday, September 14, 2009

MUZIKI BASI MPAKA MWAKANI NIMALIZE SHULE (NOORAH)

Noorah aka The Babaz of The Mamaz amelonga na Bongo Star Link na kusema kwa sasa elimu kwake ikiwa imefikia mkiani kwa Ng'ombe, ameona awaambie mashabiki wake wawe na subira kidogo mpaka hapo mwakani mwezi wa 6.
Kwa kipindi hicho chote basi amesema mashabiki wake wanaompenda wanaweza kuchukua simu zao za mkononi na kwenda sehemu ya sms na kuandika

BABAZ kwenda 15327 au NOORAH kwenda 15551.

Hapo wataweza kuwasiliana na yeye moja kwa moja kwenye simu yake ya mkononi na yeye atakuwa anawafahamisha habari mpya kuhusu maendeleo yake, it's means wao ndio watakuwa wa kwanza kujua before anyone

HUYU NDIE MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA BIG BROTHER AFRICA4

Elizabeth
Age 21
Country Tanzania
Hometown Dar Es Salaam
Occupation TV Presenter / Actress
Biography Elizabeth has one sister, two brothers and she's a Miss Tanzania Top 10 finalist. She says the best part of her country to visit is Mount Kilimanjaro and the best thing about Tanzanians is their kind and positive nature. Elizabeth is a big Man United and Chicago Bulls fan and rates sleeping late and waking up too early as her bad habits. She loves dancing, needle work, cooking, watching TV and traveling - she has also lived in Hungary.

Saturday, September 12, 2009

MASIKINI WEMA SEPUTU

Mazoea yana tabu, msemo huo upo nyuma ya adha anayoipata hivi sasa, Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kutokana na jinsi anavyohangaikia gari za kukodi wakati amezoea ‘kusumbua’ kwa usafiri wake binafsi....

Friday, September 11, 2009

AMBWENE YESAYA KUTUMBUIZA JUMAPILI HII BIG BROTHER AFRICA

Ambwene Yesaya (ay)
habari zimeingia punde zinadatisha kwamba mwanamuziki nyota wa kizazi kipya ambwene yesaya a.k.a AY anaondoka Jumamosi hii kuelekea sauzi katika jiji la johannesburg ambako atatumbuiza kwenye hafla ya Big Brother. Ataongozana na Snare wa east coast.
AY kaiambia globu ya jamii kwa njia ya twitter sasa hivi kwamba yeye kama kawaida yake hana show kubwa wala ndogo na kwamba show zote kwake ni muhimu hivyo anajiandaa kwa makamuzi ya nguvu.
kasema baada ya sauzi ataelekea Malaysia ambako atakuwa na show jijini Kuala lumpur September 24, mwaka huu ndani ya klabu cha Titunium. Pia ataporejea wiki ijayo anatarajiwa kutoa singo ingine mpya iitwayo 'Bed & Breakfast' ambayo imetayarishwa na Hermy B wa B. Hitz Studios.
Wakati huo huo AY anawakumbusha wadau wote popote walipo hapa bongo kumpa taffu kwa kumpigia kura katika tuzo za Mtv Africa. Kumpigia kura andika 'BHH AY' kisha tuma sms kwenda namba 0789 777 333

BONGO CELEBRIT YAKATA MZIZI WA FITINA


kutokana na madongo anayorushiwa supa staa steven kanumba kwa kile kinachodaiwa kuchapia kiinglishi,
WWW.BONGOCELEBRIT.COM
ambayo ni globu dada ya globu ya jamii, imeandaa clip za baadhi ya matukio katika jumba la Big Brother Africa IV akiwemo kanumba ili kukata mzizi wa fitna. ili kuona kama hayo yasemwayo ni kweli ama uzushi....
BOFYA HAPA

Thursday, September 10, 2009

TID KUSHUKA NA FILAMU YAKE INAYOELEZEA MAISHA YA JELA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava, Khalid Mohamed aka 'TID' anarejea tena kwenye medani ya filamu na kutoka na filamu yake ya Prisoner inayozungumzia maisha yake ya gerezani.
Akizungumza hivi karibuni, TID anayemiliki bendi ya Top Band, alisema kuwa ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuweka hadharani maisha wanayoishi wafungwa wawapo gerezani.

TID alifungwa kifungo cha mwaka mmoja mwaka jana kutokana na kosa la kumjeruhi mtu akiwa klabu, lakini aliweza kutoka jela kutokana na msamaha wa rais mwishoni mwa mwaka jana.

Mwanamuziki huyo ambaye amebadilika kitabia mara baada ya kutoka jela, alisema kuwa amejifunza mambo mengi alipokuwa gerezani na anahitaji kutoa elimu kwa wananchi.

"Kule gerezani nimekutana na mambo mengi yanayotisha na yanayokwenda kinyume na haki za binadamu. Nimeona kuna haja ya kuandaa filamu hii, ili wengine ambao hawajawahi kwenda jela waweze kujifunza," alisema mwanamuziki huyo.

TID ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliotoa mchango mkubwa katika medani ya filamu, hasa kutokana na ushiriki wake katika filamu ya Girl Friend, ambayo ilitoa hamasa kubwa kwa watanzania kushiriki filamu.

UNAWAJUA MAPACHA HAWA WAKO NDANI YA BBA 4


Shindano la nne la Big Brother limeanza jana jijini Johannesburg kwa mbwembwe za hali ya juu huku mabadiliko makubwa yakijitokeza kama kauli mbiu yao "mapinduzi" isemavyo.

Moja ya vivutio vikubwa katika uzinduzi wa shindano hilo ni pamoja na uhusishwaji wa mastaa wa tasnia ya filamu barani Afrika ambapo msanii Kanumba wa Tanzania aliungana na mastaa wengine watatu katika jumba hilo kuwakaribisha washiriki 11 kati ya washiriki 14 wanaotakiwa katika nyumba hiyo.
Moja ya mambo yaliyostua wadau na wapenzi wengi wa shindano hilo la Big Brother Revolution 2009 ni pamoja na kutoingia kwa washindani 3 wa nchi za Tanzania, Angola na Zambia kitendo kilichotafsiriwa na wengi ya kuwa huenda Kanumba ndiye mshiriki kamili wa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo meneja masoko wa kampuni ya Multi Choice Tanzania aliwataka watanzania kuwa na subira ili kujua hatma ya ushiriki wao.

Uzinduzi huo ambao uliongozwa na MC mahiri kabisa IK kutoka nchini Nigeria ilipambwa na burudani toka kwa K'naan na pia ilikuwa na surprise ya washiriki mapacha kutoka Namibia pamoja na washiriki mmoja mmoja zaidi kutoka Kenya na Uganda.
Aidha washiriki wote 12 walioingia ni wanaume na waliobaki inasemekana ni wanawake hivyo kuweka shauku ya hali ya juu kwa watazamaji wa shindano hilo.

KWA HILI RAISI JAKAYA AMEANDIKA HISTORIA MPYA TANZANIA


Mh Rais Jakaya Kikwete akiongea moja kwa moja na wananchi kupitia Luninga na Redio kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Tido Muhando.
Hivi ndiyo ilivyokuwa wakati Rais Jakaya alipoongea na watanzania (Live) moja kwa moja kupitia Redio na Televisheni na kuulizwa maswali mbalimabli na wananchi ili kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa yahusuyo utendaji wa serikali na matarajio ya watanzania.
Utaratibu huu umebuniwa kwa mara ya kwanza na Rais Jakaya na ni kwa mara ya kwanza toka tujipatie uhuru kutoka kwa wakoloni, Mh Rais alizungumzia mengi na kujibu maswali mengi kutoka kwa wananchi
Lakini moja ya mambo aliyozungumzia ni uhuru wa wananchi kuzungumzia na kukosoa utendaji wa serikali na akazungumzia pia uhuru wa vyombo vya habari na kusisitiza vyombo hivyo kufuata maadili ya kazi zao bila kuandika habari za uongo na uchochezi, hili ni jambo jema sana kwani tunahitaji habari nyingi zaidi lakini pia tunahitaji habari za kweli na zenye upembuzi yakinifu ili jamii iweze kupata habari zilizo sahihi
Tunakupongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wako wa kuongea na wananchi huku ukiulizwa maswali mabalimbali na kuyajibu, kwa kutendo hiki umeandika historia mpya ya uhuru wa umma kupata habari na kutoa maoni yao juu ya uendeshaji na uboreshaji wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla tunakupa Heko kwa uamuzi wako huu na tunadhani utazaa matunda, tunakutakia mafanikio mema katika kazi zako za kila siku katika kujenga Taifa letu Tanzania.

Monday, September 7, 2009

KANUMBA MMOJA WA MASTAA WATAKAOWAKARIBISHA WASHIRIKI WA BIG BROTHER AFRICA 4

kanumba,mmoja wa mastaa atakayewakaribisha washiriki wa big brother africa 4 2009 ndani ya jumba lao
Muigizaji nyota wa filamu hapa bongo, Steven Charles Kanumba(pichani)amechaguliwa kuwa mmoja wa mastaa watakao wakaribisha washiriki wa shindano la Big brother afrika 4 ,2009 nchini afrika ya kusini.Kanumba ameukwaa ustaa huo baada ya kutajwa jana kwenye hafla fupi iliofayika pale Paradise City Hotel - Savanna Lounge jiji Dar,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi rasmi wa shindano hilo,iliyoandaliwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania.
Aidha muwakilishi wa shindano hilo kwa hapa Tanzania,imeelezwa kuwa atatangazwa hapo baadaye.Tanzania imeshafanikiwa kuwakilishwa na Mwisho Mwampamba, Richard ambaye alikuwa mshindi na Latoya.
BIG BROTHER AFRICA 2009
Hatimaye lile shindalo la big brother africa limeanza tena na anaonekana msanii kanumba ndani ya jengo lile wengi wanadhani labda yeye ndio mshiriki kutoka tanzania kumbe wala hata hausiki na chochote je unajua ni ni kanumba anachokifanya ndani ya jengo hilo tulia hapahapa nitakujuza na je unamjua mshiriki halali atakayeingia ndani ya shindalo hilo basi nitakuja mengi kuhusiana na hilo

counters