Inakimbizaaaaa


Friday, April 8, 2011

Raisi Jakaya Kikwete ulituahidi barabara hii utaikumbuka

Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimeanza klusababisha kero za aina mbalimbali hasa kwa wakazi wa jijini ambao wanatoka katika maeneo yaliyo sahaulika kwa miundo mbinu. Pichani ni Barabara ya Ukonga Mombsa-Moshibar/Kwamkolemba kupitia Mazizini ambayo mbali na mahandaki na mabwa ya maji yaliyopo pale Mombasa lakini sasa barabara hiyo imeanza kuchimbika na maji yan mvua yanayo tiririka. Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni zake za kuwania urais na kufanya mkutanmo wa hadhara Kwamkolemba alitoa ahadi kwa wapiga kura wake hao kuwa pindi aingiapo madarakani barabara hiyo itaanza kujengwa.

No comments:


counters