Inakimbizaaaaa


Thursday, January 21, 2010

pati kali la kufungua mwaka,traveltine patakuwa hapatoshi jumapili hii

Mwanamama machachari kabisa ka

tika fani ya utangazaji hapa jijini Dar,Maimartha wa Jesse ameiambia JIACHIE mapema leo kuwa anatarajia kufanya onesho moja kamambe la miondoko ya ngoma za kimwambao.ak.a Taarabu.

Akizungumza kwa ucheshi mkubwa kama kawaida yake,Maimartha amefafanua kuwa onesho hilo litakuwa la aina yake na linatarajia kufanyika januari januari 24 kwenye ukumbi wa Traveltine,aliongeza kuwa onesho hilo litajulikana kwa jina la Party Kali la Kufungua mwaka 2010,ambapo wana kikosi cha Wela Wela watachuana vikali na mwanadada nguli katika miondoko ya chakacha kutoka Nairobi,Kenya,Fifii Moto

Maimartha amesema onesho hilo litawahusisha wakali wa muziki wa taarab Afrika Mashariki ambao ni Jahazi Morden Taarab, malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa na mkali wa kunengua kutoka Nairobi nchini Kenya Fifii Moto ambaye tayari yuko jijini kwa maadalizi kadhaa ya mtikisiko huo wa miondoko ya Taarab.

Aidha katika onesho hilo litakalokuwa na msisimko wa kipekee kabisa kiingilio chake kimepangwa kuwa 5000/= kwa kila kichwa,na onesho hilo limedhamiwa na redio ya Clouds Fm

NMB yatoa mashine ya kusaga kwa kinamama karatu


Mkuu wa Wilaya ya Karatu Methew Sedoyeka akishuhudia makabidhano ya mashine ya kusaga iliyokabidhiwa na benki ya NMB kwa kikundi cha akina mama wilayani karatu kama msaada wa kuendeleza biashara ndogo ndogo wanazofanya kina mama hao. Kikundi hicho kimekuwa vile vile mfano mzuri unaorejesha mikopo kwa wakati kutoka benki ya NMB.

Thursday, December 31, 2009

tanzania yajiandaa vyema na kombe la dunia 2010

aina ya bango litalotumika katika kampeni ya TTB na TFF ya kuhamasisha umma kwenda kuishangilia Taifa Stars itapocheza na Ivory Coast January 4, 2010 katika uwanja wa taifa jijini Dar

Monday, December 14, 2009

SERENGETI BREWERIES LIMITED YADHAMINI KOMBE LA NYAMAGANA KWA SH. MILLIONI 10.

Kampuni ya bia ya Serengeti leo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa waandaaji wa kombe la nyamagana la mpira wa miguu.
Ndugu Bahati Singh Mkuu wa Masoko na Utekelezaji alikabidhi hundi ya Shilingi milioni kumi pamoja na vifaa vya michezo vikiweno jezi, vikombe na medali katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika nyumbani hotel jijini Mwanza, Makabidhiano hayo ambayo yalihudhuriwa na Meneja mauzo wa kanda ya ziwa Bwana Avinash Maggirwar na Meneja Masoko kanda ya ziwa Bwana Yohana Manoli.
Akizungumza katika hafla hiyo Bwana Bahati Singh alisema’ NI heshima tele tena SBL kudhamini mashindano haya katika jiji la Mwanza kwa kuwa tuna kiwanda chetu na malengo makubwa ya SBL ni kukuza kiwango cha mpira wa miguu Nchini na pia katika mikoa ambayo tunaihudumia kijamii.
Mchango wetu wa leo ni kupitia zao la Premium Serengeti Lager tunaleta mahusiano mazuri na wanachi wa nyamagana na kuwaleta pamoja kwa njia ya mpira wa miguu na kuleta Amani, Urafiki, UPendo na Umoja kwa watu wa Mwanza.
Pamoja twaweza sema Asante kwa jamii ya watu wa Mwanza kwa kuunga mkono SBL na hii ni asilimia na kusema asante tena watu wa Mwanza.Imesainiwa na:Teddy MapundaMENEJA MKUU MAHUSIANO JAMII NA MAWASILIANO

Friday, November 13, 2009

ELIZABETH AKIFANYA MAHOJIANO NDANI YA CLOUDS FM

Pichani ni Aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta alipokuwa akifanya mahojiano Kapt Gadna G Habash kupitia kipindi cha Jahazi leo jioni kinachorushwa na redio ya Clouds Fm 88.4,shoto ni Meneja Huduma wa Multchoice Ronald Shelukindo aliyekuwa ameambatana nae.
Elizabeth amesema kuwa kwa ana mpango wa kuendelea na masomo,lakini kwa sasa anataka ajishughulishe zaidi katika mambo ya burudani ikiwemo suala la uigizaji filamu,utangazaji na mambo mengineo yanayohusiana na nyanja hiyo kwa ajili ya kujipatia kipato zaidi ili aweze kuendelea na masomo,aidha Elizabeth amesema kuwa atashukuru sana kama atajitokeza mfadhili wa kumpa sapoti katika kakamilisha safari yake ya mosomo.Eliza a,emeongeza kuwa yeye tayari ana mchumba ambaye yuko ughaibuni mambo yakiwa tayari basi kila mmoja atamfahamu.



Thursday, November 12, 2009

Zola D kuachia Hustler King


Rapa mwili nyumba, Zola D aka Unde, atazindua albamu yake ya Hustler King kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Novemba 12 kwenye usiku utakaowakutanisha vichwa vikali vya Afrika Mashariki kwenye steji moja. Uzinduzi huo unadhaminiwa na kampuni ya Aurora

Elizabeth akiongea na wanahabari

Mshiriki wa Big Brother E,izabeth Gupta akiongea na wanahabari leo hoteli ya Paradise jijini Dar. Kulia ni bosi wa operesheni wa MultiChoice Baraka Shelukindo na shoto ni afisa operesheni wa MultiChoice Grace Urassa. Pamoja na mambo mengine Elizabeth amewashukuru wadau kwa kumpigia kura na kumpa taffu katika kipindi chote alichokuwa mjengoni.
kasema ana mpango wa kurudi masomoni kwani ndio kwanza kamaliza kidato cha sita hivyo ana kiu ya kusoma sanaa na kuigiza pamoja. amesema anapenda kuigiza na kuimba na ameshawahi kuwa mtangazaji. amesema anatafuta sponsa kujiendeleza katika sanaa na akimkosa atajilipia mwenyewe.

kambi ya kisura wa tanzania mambo mswano

Washiriki wa shindano la umalkia wa Kisura wa Tanzania wakiwa na wasimamizi wao na wapiga picha wa kampuni inayoongoza kwa kazi hiyo ya Sophia Productions wakipozi kwenye magofu ya kale ya karne ya 13 yaliyopo Kaole nje kidogo ya Bagamoyo ikiwa ni mojawapo ya shughuli zao wakiwa kambini kwao hoteli ya Kiromo ambayo imewadhamini kwa mwezi mzima wa kambi. Meneja wa mradi huo Grace Kilembe ameketi wa pili shoto na anayemfuatia ni mshindi wa mwaka jana Emmy ambaye kwa sasa anafanya kazi za umodo sauzi na kaja kusaidia kazi ya kusimamia warembo hawa

Mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta arejea nyumbani


Mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta akiwasili ndani ya hotel ya Paradise huku akitabasamu Mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta akiwasili jana jioni katika uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere akitokea nchini Afrika ya kusini ambako alikuwa kishiriki shindano la Big Brother Revolution,kulia ni mama yake mzazi Bi. Hellen Gupta salaam na shoto ni Meneja huduma wa kampuni ya Multichoice Bw. Ronald Shelukindo Meneja huduma wa Multchoice
Mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta akiwa amepozi picha ya pamoja na wafanyakazi wa Paradise City Hotel jana usiku mara baada ya kuwasili toka nchini Afrika ya Kusini alikokuwa akishiriki shindano la Big Brother Africa Revolution.
Familia ya mshiriki wa Big Brother Africa Revolution Elizabeth Gupta katika uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere jana jioni wakisubiri kuwasili wa kwa mshiriki huyo.

counters