Inakimbizaaaaa


Monday, December 14, 2009

SERENGETI BREWERIES LIMITED YADHAMINI KOMBE LA NYAMAGANA KWA SH. MILLIONI 10.

Kampuni ya bia ya Serengeti leo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa waandaaji wa kombe la nyamagana la mpira wa miguu.
Ndugu Bahati Singh Mkuu wa Masoko na Utekelezaji alikabidhi hundi ya Shilingi milioni kumi pamoja na vifaa vya michezo vikiweno jezi, vikombe na medali katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika nyumbani hotel jijini Mwanza, Makabidhiano hayo ambayo yalihudhuriwa na Meneja mauzo wa kanda ya ziwa Bwana Avinash Maggirwar na Meneja Masoko kanda ya ziwa Bwana Yohana Manoli.
Akizungumza katika hafla hiyo Bwana Bahati Singh alisema’ NI heshima tele tena SBL kudhamini mashindano haya katika jiji la Mwanza kwa kuwa tuna kiwanda chetu na malengo makubwa ya SBL ni kukuza kiwango cha mpira wa miguu Nchini na pia katika mikoa ambayo tunaihudumia kijamii.
Mchango wetu wa leo ni kupitia zao la Premium Serengeti Lager tunaleta mahusiano mazuri na wanachi wa nyamagana na kuwaleta pamoja kwa njia ya mpira wa miguu na kuleta Amani, Urafiki, UPendo na Umoja kwa watu wa Mwanza.
Pamoja twaweza sema Asante kwa jamii ya watu wa Mwanza kwa kuunga mkono SBL na hii ni asilimia na kusema asante tena watu wa Mwanza.Imesainiwa na:Teddy MapundaMENEJA MKUU MAHUSIANO JAMII NA MAWASILIANO

No comments:


counters