Inakimbizaaaaa


Thursday, January 21, 2010

pati kali la kufungua mwaka,traveltine patakuwa hapatoshi jumapili hii

Mwanamama machachari kabisa ka

tika fani ya utangazaji hapa jijini Dar,Maimartha wa Jesse ameiambia JIACHIE mapema leo kuwa anatarajia kufanya onesho moja kamambe la miondoko ya ngoma za kimwambao.ak.a Taarabu.

Akizungumza kwa ucheshi mkubwa kama kawaida yake,Maimartha amefafanua kuwa onesho hilo litakuwa la aina yake na linatarajia kufanyika januari januari 24 kwenye ukumbi wa Traveltine,aliongeza kuwa onesho hilo litajulikana kwa jina la Party Kali la Kufungua mwaka 2010,ambapo wana kikosi cha Wela Wela watachuana vikali na mwanadada nguli katika miondoko ya chakacha kutoka Nairobi,Kenya,Fifii Moto

Maimartha amesema onesho hilo litawahusisha wakali wa muziki wa taarab Afrika Mashariki ambao ni Jahazi Morden Taarab, malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa na mkali wa kunengua kutoka Nairobi nchini Kenya Fifii Moto ambaye tayari yuko jijini kwa maadalizi kadhaa ya mtikisiko huo wa miondoko ya Taarab.

Aidha katika onesho hilo litakalokuwa na msisimko wa kipekee kabisa kiingilio chake kimepangwa kuwa 5000/= kwa kila kichwa,na onesho hilo limedhamiwa na redio ya Clouds Fm

No comments:


counters