Inakimbizaaaaa


Thursday, October 8, 2009

BIG BROTHER YAZIDI KUPAMBA MOTO






Baada ya mshiriki wa tanzania kwenye shindano la Bigbrother Africa kuwepo kwenye dangerzone na ikiwa ni siku ya 32 unachotakiwa ni kumpigia kura Elizabeth ili aelendelee kubaki kwenye shindano hilo na kunyakua dola za kimarekani laki mbili

BONGO STAR SEARCH KUFANYIKA JUMANNE WIKI IJAO

Mkurugenzi wa Benchmark Production Madame Rita Paulson(katikati)akiongea na waandishi wa habari juu ya kutangaza zawadi kwa washindi wa Bongo Star search(BSS)(kushoto)Brand Manager wa Kilimanjaro George Kavishe(kulia)Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania Emillian Rwejuna.Mashindano haya yatafanyika Diamond Jubilee Jumanne ijayo.
Baadhi ya washiriki walioingia katika kinyanganyiro cha kumpata mshindi wa Bongo Star Search (BSS)wakiwa wanaimba mbele ya waandishi wa habari kuonyesha vipaji vyao kabla ya shindano lao la mwisho litakalofanyika Diamond Jubilee Jumanne ijayo.Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo.

Wednesday, October 7, 2009

THE KING ON HIS WAY

yule Robert kelly"THE KING OF R&B' Anarudi na album mpya..stay tuned for more information

FIESTA ONE LOVE SASA YAELEKEA MWANZA

Fid Q ndie msanii atakaewakaribisha wenzake katika mkoa wake wa Mwanza siku ya tarehe 10 pale kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Wasanii wanaozidi 10 wanatarajia kutumbuiza siku hiyo, nadhani wanaeleweka haina haja kurudi au sio wadau.... sema Ngosha Ngosha Ngosha
Basi kama vipi nikirudi nitakuwa full madini ya kuimarisha blog yetu

ELIZABETH MSHIRIKI WA TANZANIA BBA YUKO PABAYA WIKI HII

Wiki hii Big aliwaweka katika timu ya watu wawili washishiriki wote ambapo Elizabeth yupo na Kevin mshiriki kutoka Nigeria ikimaanisha ni timu ya mtu mmoja iwapo mmoja wao akitolewa basi wote wawili wanatoka....Katika nomination jumatatu hii timu ya Kristal na Quinn pamoja na timu ya Hannington na Yakob ilikuwa up for eviction,lakini Head of the house Itai alipewa na Big jukumu la kuiokoa timu moja na kuiswap timu ingine,Itai aliwaokoa Kristal na Quinn na kuwaweka Elizabeth na Kevin for eviction this week...so tumpigie kura Elizabeth aendelee kubaki...utaratibu wa mwaka huu ni tofauti na mwaka jana mwaka huu una vote for your favourate housemate...

LEO NDIO BIRTHDAY YA RAISI JAKAYA KIKWETE


MSINISEME KAMA NAPENDA KULA

Jamani napenda kula mimi sana,kila siku nakaa naisubiria misosi..ila cha ajabu wala sinenepi...
Najitahidi sana lakini wapi sinenepi..my Boyfriend anataka niwe mnee kidogo lakini wapi..pls nisaidieni nifanye nini niwe mnene maana ntaachwa kisa wembamba...

Monday, October 5, 2009

MOVE MPYA YA KIBONGO YATOKA

Huu ndio muonekano halisi wa nakala yako utakayoinunua dukani wadau tuwe wazalendo kwa kununua nakala halisi na si fake

HUYU NDIE MISS TANZANIA 2009


Miriam akiwapungia mashabiki walioudhuria miss Tanzania ilyofanyika Mlimani City
Nasreem Karim miss Tanzania aliyepita akimvisha taji miss Tanzania wa 2009- 2010 bibiye Miriam Gerald ambaye alikuwa ni mwakilshi wa miss Mwanza

ngwea aachia ngoma nyingine

Mangwear akiwa mwishoni mwishoni kumalizia album yake itakayokwenda kwa jina la NG'E 1892, ametoa wimbo mwingine akimshirikisha Babuu wa kitaa unaokwenda kwa jina la WAR KITAA. Wimbo huu ametengenezwa pale kwa Master Jay chini ya mtu mzima Marco Chali.
USIKILIZE WIMBO HUU HALAFU UNIPE MAONI YAKO.

counters