Inakimbizaaaaa


Monday, July 4, 2011

Kitanda kinahitaji busara, siyo upole wala mapepe – 2

Jamii itambue kuwa mtu anayejifanya mpole kitandani hawezi kufanikiwa. Mwisho atamboa mwandani wake. Mantiki ya kutokuwa na muwajibikaji, hujenga tafsiri upande wa pili kwamba hujisikii inavyotakiwa, au huna hamu ila unatenda kwa kulazimisha.

Mzuka wa kutosha ni kitu muhimu mno unapokuwa faragha. Ndipo mwenzi wako anapoweza kuona mpo pamoja na akaamini kuwa unamtosheleza. Atajuaje kama anakupa raha stahiki ikiwa mwenzako anawajibika wewe umetoa macho kama mjusi kabanwa na mlango?

Hivyo basi, busara ya kwanza ya kitanda iwe ni kuziweka hisia zako kwenye tendo. Akikushika nawe shikika. Usizuie hisia, hebu tekenyeka basi. Unajikausha ili uonekane mgumu, nani alikwambia ugumu una nafasi pale wawili wanapokutana faragha?

Ukweli ni kuwa sanaa ya mapenzi inamuongoza mtu kujua maeneo gani ya kufanyia kazi. Kwa maana mpenzi wako atataka ayabaini maeneo ambayo wewe hukupa mzuka wa kutosha. Sasa atayajuaje kama unajikausha. Unaguswa mahali, wewe unakakamaa mwili mzima ili usioneshe hisia.

Ni mapenzi siyo mateso. Ni mchezo wa kugawana hisia. Mgawie zako naye akugawie zake. Usizibane, ukifanya hivyo utafeli. Mpe urahisi wa kutambua maeneo ambayo yanaweza kukupa raha, naye afanye hivyo kwako ili muweze kwenda sawa.

EPUKANA NA AIBU HII
Mtu bora ni Yule anayechukua muda kufika mshindo mmoja, halafu anapumzika kwa muda wa kutosha kabla ya kurejea ulingoni tena. Umekutana naye, mara dakika tatu umecheua, kabla hujajipanga unataka upande tutani tena. Utachekwa kila siku.
Mapenzi hayakuumbwa ili umkomoe mwenzako.

Itaendelea wiki ijayo.

No comments:


counters