Inakimbizaaaaa
Saturday, June 25, 2011
Vimwana wa Twanga Pepeta wako tayari kwa Fainali
Washiriki wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 wameiva na wako tayari kwa ajili ya Fainali za Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 zinazotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Ijumaa tarehe 08-07-2011. Vimwana hao ambao wameongezewa Mwalimu wa kuwafundisha kucheza ili waweze kufanya vizuri katika Fainali za Shindano hilo. Hapo awali walikuwa wakifundishwa na Kassim Mohammed au "Super K" lakini kwa sasa wameongezewa mwalimu atakayesaidiana naye ambaye ni Bakari Kisongo aka "Mandela". Washiriki walioingia Kumi Bora kama wanavyoonekana kwenye picha ni pamoja na Leila Mshana, Mary Hamis, Mariam Mwakyoma, Amina Juma, Hawa Miraji, Amanda Cyprian, Rehema Said, Johari Juma, Edina Amani na Salha George. Mshindi atakayeibuka Mshindi atajinyakulia zawadi ya Duka la Vipodozi lililogharimu kiasi chaa shilingi milioni tano ambalo lishapatikana lipo Kinondoni Studio jirani na kituo cha Daladala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment