Wiki mbili zilizopita niliwaletea makala kuhusu soya ambapo tuliona kuwa maziwa yatokanayo na zao hilo wanayopewa watoto siyo salama kiafya. Hali kadhalika bidhaa nyingine zitokanazo na soya zinaweza kuwa na madhara kiafya kwa mtu yeyote iwapo zitaandaliwa kinyume na inavyotakiwa.
Wiki hii tuangalie ni kwa kiasi gani maji ni tiba kubwa kuliko zote mwilini. Mwili wa binadamu unategemea maji kwa kiasi kikubwa na unapokosa au kupungikiwa, hutoa ishara zake ambazo wengi wetu hatuzijui. Ishara hizo zinapopuuzwa huzaa matatizo mengine ya kiafya.
Kwa uchache, binadamu anatakiwa kunywa maji yasiyopungua glasi nane kila siku. Kiwango hicho kitaongezeka iwapo mtu ana uzito mkubwa na shughuli zake nyingi zinatumia maji mengi…
No comments:
Post a Comment