Inakimbizaaaaa


Thursday, January 28, 2010

WANAOTUHUMIWA KUMUUWA SWETU MAHAKAMANI


Watuhumiwa wa Kesi ya Mauaji ya mtoto wa Chifu Fundikira, ambao wanaaminika kuwa ni Watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) (kushoto) na MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kusomewa mashitaka yao ya ambapo wawili hao wanadaiwa kumshambulia kwa kumpiga hadi kusababisha kifo cha Swetu Fundikira huko Kinondoni katika barabara ya Mwinjuma jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo vyanzo kadha vya blogu hii ya jamii vinasema kuwa watu hao ambao si wanandoa pia Ngumbe si askari wa JWTZ Kikosi cha Lugalo bali wote ni kutoka JKT Mbweni.

No comments:


counters