Inakimbizaaaaa


Monday, November 9, 2009

nini kimesababisha maisha club kuungua leo?

askari wa zimamoto wakipambana na moto uliokuwa unateketeza maisha club ya ostabei jijini dar mapema leo. hakuna aliyedhurika na janga hili ambalo chanzo chake bado kujulikana, japo redio mbao zinataja hitilafu zilizotokana na umeme.
sehemu yote ya mbele ya maisha club imeteketea
mama hellen sweya, mmiliki wa maisha club, akifarijiwa

Mmiliki wa kiota cha maraha Maisha Club,Mama Hellen Sweya (kati) akipewa pole na baadhi ya marafiki zake waliofika kwenye eneo la tukio leo jioni Masaki jijini Dar.Kwa picha zaidi bofya Michuzi Jr

MWAKA WA WASOMI MISS UTALII TANZANIA 2009/2010


Katika kile kinachoonekana kukubalika zaidi kwa wasomi zaidi, kiu ya Wasomi kujitoa Muhanga kwa kuutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania, wasomi wengi mwaka huu wamemejitokeza kushiriki katika mashindano ya Miss Utalii Tanzania, na kutwa mataji karibu yote katika ngazi mbalimbali za mikoa,Wilaya, na Kanda ambazo tayari zimekwisha fanya mashindano yake mwaka huu.

kama ilivyokuwa katika shindano la Miss Utalii temeke 2009, ambapo mrembo mwenye Digrii ya Uhasibu na Utawala wa Fedha Erica Allan, alipotwaa taji la Miss Utalii Temeke 2009/2010, jana Msomi mwingine mwenye shahada ya Sayansi ya Komputa, Shaymaa Ntetema aliweza kutwaa taji la miss Utalii Ilala 2009/2010 katika fainal iliyofanyika katika ukumbi wa Da' West Park Inn Tabata, Dar es Salaam.

Huku mwanafunzi wa Digrii ya Sayansi ya Jamii katika chuo Kikuu Shiriki cha Sayansi ya Jamii (Ustawi wa Jamii) Kijitonyama , Aghata Kilala aliweza kutwaa nafasi ya Pili akifutiwa na Sheila Bahamary , Mwanafunzi wa Shahada ya Juu ya Uhandishi wa Habari katika chuo cha DSJ. nafasi ya nne ilitwaliwa na Tausi Thomasi mwenye Elimu ya Kitato cha Sita huku nafasi ya tano na taji la kipaji likitwaliwa na Mwanafunzi wa Kozi za awali za Komputa, Jamida Abdu.ambapo katika shindano hilo warembo wote walipita kwa mavazi mbalimbali likiwemo la Asili ambalo pia walilitumia kama ngao ya Asili kwa kuchezea ngoma ya tamaduni za makabila ya Tanzania.

Aidha warembo waliweza kujibu maswali mbalimbali yanayohusiana na Utalii, Mila na Desturi, Vivutio vya Utalii na Hifadhi za Taifa za Utalii, Mikoa na Tamaduni mbalimbali, ikiwemo kuimba nyimbo za Tanzania. washiriki wengine walioingia katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Tickey Lithon, Frola Nicholuas, Janneth Samson, Edna Endrew, Nezia Mangaka, ambapo shindano hilo lilipambwa na wanamuziki wengi wakiwapo bendi ya Extra Bongo chini yake ally Choki, Zia Musiki, Kundi la Muziki la Ngoma za Asili, Mfalme Bendi chini yake Costar Siboka, pamoja na wanamuziki wa Kizazi Kipya, Abubakary Msasu(Kiboot) ambaye hata hivyo alichelewa kuingia Ukumbini.

kwa mujibu wa Waandaaji wa mashindano hayo, sasa shindano ambalo linatazamiwa kufana kwa aina yake ni shindano la Miss Utalii Kinondoni, ambalo limesheheni wasomi wengi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali ikiwemo, chiuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mzumbe, IFM, CBE, na Vingine Vingi Mgeni Rasmi katika Shindano hilo alikuwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mwantumu Mohamed, huku wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Mlonge by Makai Enterprises wakiweza kukabidhi zawadi kwa washindi zilizokabidhiwa na Afisa Utamaduni wilaya ya Ilala Shani Mohamed.

Saturday, November 7, 2009

Richmond yawekwa Kiporo...


HOJA nyingi za msingi zikiwamo za Richmond, Kiwira, TRL, maji ya mto Tighite na
TICTS, ambazo taarifa zake Serikali iliahidi kuwa ingeziwasilisha katika Bunge
lililoahirishwa jana, zimebaki kiporo...

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Waandishi wa habari,Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi kwa lengo la kuweka rekodi sawa.
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikituhumiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwamba mimi si Mwanachama wa Chama hicho na kwamba sitoi misaada ya hali na mali kwa Chama Cha Mapinduzi.Ndugu Wanahabari,Kwa msemo wa kiingereza“Don’t argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool”,wenye maana kwamba usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga!Hata hivyo wakati mwingine inakulazimu kujibu hoja unapomwona mtu anapotosha mambo kwa makusudi.
Kwanza,kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi.Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili.Pili,kuhusu uwanachama wangu wa CCM:Napenda kuwaambia kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni Na.B124595, iliyotolewa na Tawi la Kisutu,Wilaya ya Ilala,Mkoa wa Dar es Salaam.Hivyo basi madai yote kwamba mimi si mwanachama au nilijiunga na chama hivi majuzi kama inavyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba,Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Shaaban Kilumbe Ng’enda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM John Guninita ni uongo,uzushi na umbea wenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wanachama za kupiga ufisadi vita.Mimi na wenzangu wengine tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba chama chetu kinaongozwa katika misingi yake ya asili ya kupiga vita rushwa na maovu mengine.Ndugu Wanahabari,Hawa wanaodai kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi msafi ni wazi kwamba wamedandia chama hiki hivi majuzi.Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM.Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza.Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.Aidha,ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.Reginald A. MengiMWENYEKITI MTENDAJI,IPP LTD

AMA KWELI MCHINA HANA DINI HIVI WASANII WETU WATAFIKA KWELI?





Pichani ni sehemu ndogo tu ya Cd feki zinazosambaa mitaani na kuuzwa,zenye filam kumi kwa moja amboa nyingi zimekamatwa Arusha,Mwanza na Dar es Salaam. Vile vile zimetapakaa mpaka Congo na Nchi jirani.Je? Wasanii tutafanikiwa kwa hali hii?Watanzani wenzangu kazi tunazofanya ni ngumu sana lakini wanaofaidika ni watu ambao hawatumii nguvu kubwa.Ombi letu kwa Watanzania wote mlio nje ya nchi na ndani ya nchi msinunue kazi zenye mfano wa makava haya.
Wanajamvini imefika mahali jamani tuwaonee huruma wasanii wetu wa filamu hapa bongo, kusema ukweli wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuhusiana na uharamia wa kazi zao unaozidi kukithiri kila kukicha,wanawekeza muda wao mwingi,fedha zao na mambo chungu mzima lakini wanaokuja kufaidika ni mtu/watu baki kabisa ambaye kimsingi hakupaswa kufaidika,Jamii inatupasa kumka sasa kupambana na hii vita ingawa ni ngumu lakini angalau basi tuoneshe moyo wa kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine,Vingnevyo wasanii wetu watakuwa masikini kila siku huku tukiwacheka na kuwauliza kwa nini hawaendelei,wakati majibu ya tatioz tunayo

KOMBE LA BARCLAYS LATUA BONGO



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Rished Bade, wakilinyanyua juu Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza la Barclays , katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya kuwasili Dar leo.

benefit concert in columbus, ohio, november 21, 2009


In an effort to help my fellow Albinos in Tanzania improving their overall wellbeing; Nov 21st from 11pm, Tanzanian, Kenyan, and Zambian Artists from all over the states will be joining me for a BENEFIT CONCERT in Columbus, OH.
All proceeds go to purchase sunscreens for kids ages 5-10 in an exertion to prevent skin cancer. Please Join us to make this happen!!!
-- +255 717 705320
+255 756 610100
KARIBUNI SANA WOTE
ALBINO FULANI
http://www.babkubwa.com/
http://www.babkubwa.ning.com/
www.myspace.com/michael_mlingwa

Friday, November 6, 2009

VODACOME MISS TANZANIA MIRIAM GERALD AKABIDHIWA UWAKILISHI WAKE RASMI

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi bendera ya Taifa Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald, mrembo huyo anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika tarehe 12 mwezi Disemba mwaka huu katika mji wa Sanddown nchini Afrika Kusini na ataondoka kesho (leo) kuelekea nchini humo ili kujiunga katika kambi ya Miss World pamoja na warembo wengine wanaowakilisha nchi zao.

NI WEB YA MAWASILIANO KAMA VILE HI5 FACE BOOK MY SPACE


mimi ni mtanzania ninaishi moscow kimasomo....nina webu ya mawasiliano like hi5,myspace,facebook yaani mtandao wa kuwasiliana.N
Naomba uniwekee hewani watu waione http://www.kislat.com/.kislat(Keep Insight Love All Times) nimtandao unaowakutanisha watu wote popote walipo duniani.(kislat is a social network website which connect you with the rest of the world,upload photos,video,forums,create and join groups,create post and videos,meet old and new friends!!!).
.Shukrani sana,God Bless You.

ALLI CHOKI, MAC DEE KUPAMBA MISS UTALII ILALA LEO


Kivumbi cha kumpata mrembo wa Fainali za Miss Utalii Ilala 2009 ni tarehe 6/11/2009 Ijumaa katika ukumbi wa Da’ West Park Inn Tabata, ambapo jumla ya Warembo 12 watapanda katika jukwaa kuchuana kuwania taji kwa musimu wa 2009/2010.

Katika shindano hilo ambalo macho na masikio kwa wakazi wa Dar es Salaam limewatia wazimu kutokana na kutoelewa nani hataibua nderemo, Vifijo, na makelele kutokana na warembo wote kuwa katika hali ya Ushindani mkali ambapo kila mrembo amejigamba kuibuka na taji hilo kasha kubeba vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha thamani yake ikiwa ni milioni mbili .

Warembo hao walioanza kambi kwa takribani mwezi mmoja katika Ukumbi wa Da’ West Park Inn-Tabata, waliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii unaopatikana Tanzania ikiwemo Hifadhi za Utalii za Taifa, Vivutio vya Kitalii, pamoja na Maajabu ya Dunia yanayopatikana hapa Tanzania. Aidha katika shindano hilo, warembo hao wataonyesha Mavazi ya asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania, watacheza ngoma kuonyesha utamaduni wa Mtanzania, Watavaa mavazi ya Kitanzania ya Kitalii, vazi la Ubunifu lililotengenezwa kwa maligafi za hapa Tanzania, pamoja na mengine mengi yanayohusiana na masuala ya Utamaduni wa Mtanzania.

Warembo wanaowania taji la Miss Utalii Ilala 2009 ni pamoja na ,Tickey Lighton,Neema King’aka, Edna Endrew, Frola Nicholaus, Sheila Baamary, Janeth Samson, Nezia Gabriel, Roselina Sekwao, Jamida Abdu, Aghata Kilala, Tabus Thomas, na Shaymin Ntemena. Zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni kumi zitatolewa kwa washindi na washiriki, ikiwa ni pamoja na Fedha, na vifaa mbalimbali vyenye thamani mbalimbali, zitalolewa kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza kwa mujibu wa Waandaji wa shindano hilo ni thamani ya shilingi milioni 2, mshindi wa pili thamani ya million moja na laki mbili ,mshindi wa tatu thamani ya laki nane na , mshindi wa nne na tano, thamani ya laki tano na mshindi wa Kipaji (Talent) ni thamani ya laki saba na nusu na kifuta jasho kwa wote ni shilingi elfu thelathini na watapatiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki moja kila mmoja.

Miss Utalii Ilala katika Msimu huu ilipata bahati ya Kuungwa Mkono kwa asilimia mia moja na Mkurugenzi wa Chicken Hut Tanzania ltd ya Mlimani City, Savannah Lounge- Paradise City Hotel iliyopo katika jingo la Benjamini Mkapa Tower-Posta Mpya, Chaga Bite iliyopo Kijitonyama, Kampala International University iliyopo Gongolamboto, pamoja na Ukumbi wa Da’ West Park Inn- Tabata.

Wadhamini wengine waliojitokeza kuunga mkono ni wadau wa Shindano la Miss Utalii ikilinganishwa na miaka ya nyuma, ambapo baadhi ya watu mbalimbali wamejitokeza kusaidia ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Ulinzi na Usafirishaji ya Aurora, Kampuni ya Usafirishaji ya Mamaa Sakinma Trans, Mashujaa Pub, Kampuni ya Uongozaji Watalii na Usafirishaji Watalii ya Aucland Tours & Safari, Hotel ya Kisasa ya Grand Villa Hotel iliyopo Kijitonyama, Gym Ya kisasa ya Fitness Centre ya Chang’ombe (Oil Com), Saloon ya Kisasa ya Dage Saloon iliyopo Sinza, Kampuni ya Vifaa vya Umeme ya Vam General Suplay, Kampuni inayojishughulisha na Mti wa Maajabu Ya Mlonge(Mlonge by Makai Enterprises) na Wabunge wa jiji la Dar es Salaam Burudani mbalimbali zitapatikana katika kupamba Onyesho hilo ikiwa ni pamoja na Kundin la Muziki la Extra Bongo chini ya Ally Choki, Zia Musica,kundi la ngoma za asili Mfalme Bendi chini ya Costa Siboka zamani Mr Ginnes, na makundi mbalimbali ya muziki wa ngoma za asili, mwanamuziki wa kizazi kipya mtanzania anayeishi nchini afrika kusini Abubakari Ally (Kiboot) ambapo wote mnakaribishwa Da’ West Park Inn Tabata.

counters