Inakimbizaaaaa
Monday, November 9, 2009
MWAKA WA WASOMI MISS UTALII TANZANIA 2009/2010
Katika kile kinachoonekana kukubalika zaidi kwa wasomi zaidi, kiu ya Wasomi kujitoa Muhanga kwa kuutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania, wasomi wengi mwaka huu wamemejitokeza kushiriki katika mashindano ya Miss Utalii Tanzania, na kutwa mataji karibu yote katika ngazi mbalimbali za mikoa,Wilaya, na Kanda ambazo tayari zimekwisha fanya mashindano yake mwaka huu.
kama ilivyokuwa katika shindano la Miss Utalii temeke 2009, ambapo mrembo mwenye Digrii ya Uhasibu na Utawala wa Fedha Erica Allan, alipotwaa taji la Miss Utalii Temeke 2009/2010, jana Msomi mwingine mwenye shahada ya Sayansi ya Komputa, Shaymaa Ntetema aliweza kutwaa taji la miss Utalii Ilala 2009/2010 katika fainal iliyofanyika katika ukumbi wa Da' West Park Inn Tabata, Dar es Salaam.
Huku mwanafunzi wa Digrii ya Sayansi ya Jamii katika chuo Kikuu Shiriki cha Sayansi ya Jamii (Ustawi wa Jamii) Kijitonyama , Aghata Kilala aliweza kutwaa nafasi ya Pili akifutiwa na Sheila Bahamary , Mwanafunzi wa Shahada ya Juu ya Uhandishi wa Habari katika chuo cha DSJ. nafasi ya nne ilitwaliwa na Tausi Thomasi mwenye Elimu ya Kitato cha Sita huku nafasi ya tano na taji la kipaji likitwaliwa na Mwanafunzi wa Kozi za awali za Komputa, Jamida Abdu.ambapo katika shindano hilo warembo wote walipita kwa mavazi mbalimbali likiwemo la Asili ambalo pia walilitumia kama ngao ya Asili kwa kuchezea ngoma ya tamaduni za makabila ya Tanzania.
Aidha warembo waliweza kujibu maswali mbalimbali yanayohusiana na Utalii, Mila na Desturi, Vivutio vya Utalii na Hifadhi za Taifa za Utalii, Mikoa na Tamaduni mbalimbali, ikiwemo kuimba nyimbo za Tanzania. washiriki wengine walioingia katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Tickey Lithon, Frola Nicholuas, Janneth Samson, Edna Endrew, Nezia Mangaka, ambapo shindano hilo lilipambwa na wanamuziki wengi wakiwapo bendi ya Extra Bongo chini yake ally Choki, Zia Musiki, Kundi la Muziki la Ngoma za Asili, Mfalme Bendi chini yake Costar Siboka, pamoja na wanamuziki wa Kizazi Kipya, Abubakary Msasu(Kiboot) ambaye hata hivyo alichelewa kuingia Ukumbini.
kwa mujibu wa Waandaaji wa mashindano hayo, sasa shindano ambalo linatazamiwa kufana kwa aina yake ni shindano la Miss Utalii Kinondoni, ambalo limesheheni wasomi wengi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali ikiwemo, chiuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mzumbe, IFM, CBE, na Vingine Vingi Mgeni Rasmi katika Shindano hilo alikuwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mwantumu Mohamed, huku wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Mlonge by Makai Enterprises wakiweza kukabidhi zawadi kwa washindi zilizokabidhiwa na Afisa Utamaduni wilaya ya Ilala Shani Mohamed.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment