Shaggy akiwaimbisha maelfu ya watu waliofurika kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,ndani ya viwanja vya Carnivo jijini Nairobi,usiku wa kuamkia leoClouds Enertainment Media Group ni moja ya kampuni ambazo zinafanya vizuri sana sasa hivi katika nyanja za kuandaa matamasha ya muziki na burudani nyingine nchini Tanzania na imefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwani kuleta wanamuziki kutoka pande mbalimbali za dunia na kuonyesha uwezo wao katika kutangaza muziki wa ndani ya nchi na wa nje pia pamoja na wanamuziki wenyewe, lakini pia kampuni hii imetangaza zaidi jina lake kupitia tamasha la Serengeti Fiesta ambalo hufanyika kila mwaka lishirikisha wanamuziki wa nje ya Tanzania na ndani pia Kwa sasa Clouds Enertainment Media Group imevuka mipaka na kuratibu tamasha kubwa la muziki lililokwenda kwa jina la Tusker All Stars Concert 2011 lililofanyika jana Carnivo jijini Nairobi nchini Kenya, likishirikisha wanamuziki wakubwa kutoka Marekani na Afrika kama vile Shaggy, Eve E, na Cabo Snoop kutoka nchini Agola pamoja na wanamuziki kadhaa kutoka hapa Afrika Mashariki, ambapo tamasha hilo limefanikiwa sana na kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki huku jina la Kampuni hiyo liliendelea kujijengea heshima kubwa katika Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla Jana pamoja na kuwepo kwa hali ya mvua mvua,lakini maelfu ya watu waliokuwa kwenye viwanja vya carnivo kujiachia ndani ya tamasha la Tusker All Stars 2011,hawakutaka kubanduka kabisa,badala yake walikuwa wakijifunika na viti ili wasikose uhondo uliokuwa ukiendelea kutolewa jukwaani. Mmoja wa madada wakali katika miondoko ya hipo hop nchini Marekani,Eve E akiwaachia mistari wakazi wa Nairobi,ambao wengi wao walikuwa wakivutiwa nae kwa namna ambavyo alikuwa akionesha kukomaa kwake kwenye anga ya muziki wa hip hop. Shaggy ni mmoja wa wanamuziki ambao kiukweli awapo jukwaani hana masikhara kabisa na uwanja wake,kila wakati hupenda kuhakikisha watu wanashangweka tu,na ndivyo ilivyokuwa kwenye shoo yake usiku wa kuamkia leo,kila wakati alikuwa akiwaimbisha mashabiki nao bila hiyana walikwenda nae sambamba,hali iliyomfurahisha zaidi.
Shaggy na bak voko wake wakilishambulia jukwaa,huku maelfu ya mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakipaga mayowe kuonesha kuwa wanakunwa vilivyo na umahiri wa wanamuziki hao.
No comments:
Post a Comment