Picha ya kwanza juu Miss Sinza 2011, Felester Philip (katikati), akiwa na mshindi wa pili, Naomi John (kushoto), na mshindi wa tatu Husna Mauld muda mfupi baada ya kutajwa mshindi.
Picha inayofata Miss Sinza aliyemaliza muda wake, Amisuu Malki, akiwapungia mkono wa kheri mashabiki, muda mfupi kabla ya kukabidhi taji hilo.
KUFUATIA Kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Miss Sinza mwaka huu, Fellister Philip, ndiye aliyeibuka kidedea akiwamwaga warembo zaidi ya 15 aliyokuwa akichuwana nao kuwania taji hilo, Mtandao huu ulishuhudia.
Tukio hilo la kumsaka Mlimbwende wa Sinza lilishuhudiwa hatua kwa hatua na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Vatcan City Sinza jijini Dar es Salaam, muda mfupia baada ya harakati za kuwasaka vimwana hao kuanza.
Akizungumza na mwandishi wetu, Fellister alisema kuwa hakuwa na matumaini kabisa ya kunyakuwa taji hilo na kwamba alikuwa akimhofia sana mrembo aliyeshika namba tatu, Husna Mauld kufuatia uelelwa wake tangu alipokuwa kwenye mazoezi.
Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya Mapacha Watatu, na makundi mawili ya Kusheki kutoka Sinza huku mgeni rasmi wa Kinyang’anyiro hicho akiwa ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.
No comments:
Post a Comment