Inakimbizaaaaa


Saturday, March 19, 2011

SERIKALI YAKANUSHA UVUMI KUHUSU WAZIRI MAGUFULI YASEMA HAJAJIUZULU


SERIKALI imekanusha uvumi potofu ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli amejiuzulu kuwa si za kweli .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la serikali kufuatia uvumi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango alisema habari hizo si za kweli na Waziri Magufuli anaendelea na jukumu alilopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete .
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa na Katibu Mkuu huyo, kufuatia baadhi ya magazeti ya leo(jana) ambayo ni Tanzania Daima kuandika kwamba “Magufuli ajiuzulu “ na Nipashe limeandika “ Magufuli azushiwa kujiuzulu”

“Tunataka kuchukua nafasi hii kuwaarifu na kuwahakikishia kwamba taarifa hizi si za kweli .Mheshimiwa Waziri anaendelea na kazi zake vizuri, amekuwepo ofisini jana na leo, na anaendelea na programu zake kama kawaida .” alisema Katibu Mkuu Mrango.

Aidha Katibu Mkuu huyo, aliongeza kwamba Waziri Magufuli hajajiuzulu , hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu ya kujiuzulu.Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz

No comments:


counters