Inakimbizaaaaa


Thursday, January 28, 2010

clouds fm yasaidia kuhamasisha kampeni ya Vodafone red alert



Pichani shoto ni watangazaji wa Clouds Media Group,Hamis Mandi a.k.a B 12 pamoja na Fatma Hassan a.k.a Fetty wakiendesha harambee hiyo leo.

Kampuni ya Clouds Media Group leo inaendesha harambee ya Vodafone Red Alert inayohamasisha kuchangia waathirika wa maafa nchini. Kama unachochote kile kwa hali na mali unaweza ukaleta hapa mjengoni utakuwa umeishachangia ndugu zetu wanaoteseka.

Clouds Media Group inasaidia kuendesha zoezi hilo la kuwasaidia ndugu zetu wanaoteseka kwa kuhakikisha kiasi cha shilingi milioni 50 zinakusanywa ili kusaidia maafa hayo.

Ili kuchangia harambee hiyo unatuma sms kwenda namba 15599 na kuandika neno 'Maafa' utakuwa umeshachangia ndugu zetu wanaoteseka.

Kufuatia harembee hiyo kuanza leo tayari watu kibao wamekwishaanza kujitolea kwa hali na mali,wakiwemo wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya alias bongofleva. Ofisi za Clouds Media Group zipo Mikocheni,njia panda ya Cocacola kama unakwenda Kawe.

No comments:


counters