Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Dr.Ibrahim Msengi akipokea msaada wa vifaa vya afya kutoka kwa mkurugenzi wa Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba.Vifaa mbalimbali vya afya vyenye thamani ya Milioni 20 vilitolewa kwa hospitali ya Bombo Mkoani Tanga.Sherehe hizo za makabidhiano zilifanyika mwanzoni mwa wiki hospitalini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Tanga mjini Mh Dr.Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa vifaa vya afya kwa mganga mkuu wa hospitali ya Bombo Dr.Adam Mtatifikolo.Msaada huo ulitoloewa hospitalini hapo na kitengo cha misaada cha kampuni ya simu ya Vodacom.Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Bi Mwamvita Makamba.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya Bombo mkoani Tanga wakifurahia msaada wa vifaa vya afya vilivyotolewa na Vodacom foundatuion hospitalini hapo.Wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Dr.Ibrahim Msengi (katikati). Sherehe hizo za makabidhiano zilifanyika mwanzoni mwa wiki hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment