
SIJAACHA KAZI CLOUDS FM ILA.... MASSOUD KIPANYA

Hakuna ubishi kwamba kipindi cha PowerBreakfast kinachorushwa na radio ya Clouds FM ni mojawapo ya vipindi vya radio vyenye wapenzi na wasikilizaji wengi nchini Tanzania.
Hivyo basi haishangazi kwamba hivi karibuni watangazaji wawili wa kipindi hicho waliokuwa wamezoeleka,Masoud Kipanya(KP) na Fina Mango, walipopotea hewani maswali mengi yaliibuka.Wako wapi KP na Fina?Maoni na e-mails zikarushwa kwetu tukiombwa kuwatafuta na kujua nini kimetokea na kama wapo likizo tu au inakuwaje?
Wakati tukifanya juhudi za kujua nini kimetokea,blog maarufu ya Michuzi ikaandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari Fina Mango na Masudi Kipanya niaje?Mjadala ukazuka.Kwa bahati nzuri,nasi tukawa tumebahatika kumpata mhusika mmojawapo yaani Masoud Kipanya(KP) ambaye hakusita kutupa yake machache kuhusu nini kimetokea au kilitokea,yuko wapi,anafanya nini nk.Anasisitiza kwamba nia yake ni kutoa ufafanuzi(kwa upande wake) ili watu wasiendelee kujenga picha ambazo pengine hazitakiwi kujengwa wala hazipo.
Je PowerBreakfast ya Masoud na Fina ndio imefikia kikomo? Je ni kweli kwamba masuala ya mshahara ndio yamesababisha wapotee hewani?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi;
BC: KP,kwa muda wa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na tetesi,minong’ono,udaku nk kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwenu katika kipindi chenu maarufu cha PowerBreakfast kupitia CloudsFM.Hivi leo,blog ya Michuzi(bila shaka umesoma kilichoandikwa) iliweka kidogo kuhusiana na kilichokuwa kinazungumzwa mitaani. Je ukweli uko wapi? Upo au haupo tena katika PowerBreakfast?Nini kimetokea?
(more…)
No comments:
Post a Comment